Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Njaa yaweka rehani ubunge wa Zitto
Habari za SiasaTangulizi

Njaa yaweka rehani ubunge wa Zitto

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT na mbunge wa Kigoma Mjini
Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge pekee wa chama hicho ametangaza kujiuzulu ubunge wake iwapo serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), itathibitisha kuwa akiba ya chakula inayofikia tani milioni 1.5, anaandika Charles William.

Zitto ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini ametoa msimamo wa kujiuzu kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Facebook na Twitter.

“Serikali ya CCM ikinionesha tani 1.5 milioni za chakula ambazo inataka kusambaza, najiuzulu Ubunge mara moja. Narudia, mpaka Oktoba 2016 kulikuwa na nafaka tani 90,400 tu kwenye maghala yote ya NFRA.

“Tunashukuru kuwa Hivi sasa ajenda ya tishio la njaa inapata majawabu na matamko. Ndio wajibu wa vyama vya siasa. Kuibua masuala muhimu kwa nchi yetu,” ameandika Zitto.

Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli imekuwa ikisisitiza kuwa taifa halijakumbwa na njaa na hakuna chakula cha msaada ambacho serikali itakipeleka kwa wananchi, bali wananchi wafanye kazi kwa bidii ili kujipatia kipato halali.

Hata hivyo, katika baadhi ya maeneo ya nchi, zimeripotiwa taarifa za kuwepo kwa uhaba wa chakula unaotokana na ukame kiasi cha kusababisha vifo vya mifugo kwa kukosa malisho.

Jana Waziri Mkuu Majaliwa Kassim aliwaeleza waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa kuna akiba ya chakula inayofikia tani 1.5 milioni ambazo tayari wameruhusu zisambazwe katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili kuuzwa katika maeneo mbalimbali na kudhibiti kupanda kwa bei.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!