Thursday , 18 April 2024
Habari za Siasa

Chadema, CCM vyaonywa

Dk. Steven Kebwe, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
Spread the love

VYAMA vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Kiwanja cha Ndege, Manispaa ya Morogoro vimeonywa, anaandika Christina Haule.

Vyama hivyo vimetakiwa kujiepusha na vitendo vya vurugu wakati huu wa kampeni za udiwani zinazotarajiwa kukoma tarehe 21 Januari mwaka huu ambapo tarehe 22 Januari uchaguzi utafanyika.

Wito huo umetolewa na Dk. Steven Kebwe, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana.

Amesema kuwa, mkoa huo hautavumilia kuona chama chochote kinakiuka masharti ya uchaguzi huo kwa namna yoyote ile.

Dk. Kebwe amewashauri wananchi kuwa watulivu katika kipindi cha kampeni na kuwataka kusikiliza maelezo yanayotolewa na vyama vyote ili waweze kuchagua kiongozi watakayemuona anafaa kuwaletea maendeleo ya kweli.

Wakati huohuo Dk. Kebwe amesema kuwa, zoezi la upigaji chapa mifugo linatarajiwa kuanza kufanyika tarehe 1 Februari mwaka huu baada ya mwanzo kusitishwa kutokana na jamii ya wafugaji kutoa ushirikiano wa kutosha na baadhi ya mifugo kudaiwa kuumia kutokana na chapa hizo.

“Zoezi hili ni utekelezaji wa agizo la waziri mkuu kwa barua kumbukumbu namba PM/P/2/569/42, hivyo tunaomba ushirikiano toka kwa makundi yote, ndugu zetu wafugaji na wananchi wote wa mkoa wa Morogoro,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia atua Uturuki kwa ziara ya siku 5

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano amewasili nchini Uturuki kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia arejesha mikopo ya 10%, bilioni 227.96 zatengwa

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amerejesha utaratibu wa utoaji mikopo...

Habari za Siasa

Rais Samia amfariji mjane wa Musa Abdulrahman

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne amempa pole Mwanakheri Mussa...

error: Content is protected !!