Saturday , 13 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Njaa yaitoa mafichoni serikali
Habari za SiasaTangulizi

Njaa yaitoa mafichoni serikali

Ghala la Taifa la chakula
Spread the love

MKUBWA hasutwi. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Serikali ya Rais John Magufuli kuruhusu tani milioni 1.5 za chakula kilichokuwa kimehifadhiwa kianze kuuzwa ili kukabiliana na kupanda kwa bei, anaandika Mwandishi Wetu.

Kupanda kwa bei ya chakula kunatokana na maeneo mengi kukubwa na upungufu wa chakula kunatokana na nchi kukumbwa na ukame.

Hata hivyo, serikali imekuwa ikiwaaminisha wananchi kwamba, kuna chakula cha kutosha nchini na kwamba, wafanyabiashara ndio wamekuwa wakiendesha kampeni ya kuwepo kwa upungufu wa chakula.

Wakati serikali ikiendesha kampeni ya ‘kipo chakula cha kutosha’ jana Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu ameruhusu tani milioni 1.5 kutoka kwenye ghala na kaunza kusambazwa nchini ili kukabiliana na kupanda kwa bei ya vyakula.

Waziri Majaliwa ametoa kauli hiyo mbele ya Waandishi wa Habari muda mfupi baada ya kuwasili na ndege ya Bombadier mjini Dodoma ikiwa ni safari ya kwanza ya kibiashara kati ya Dar es Salaam na mji huo.

Amedai kuwa, mfumuko wa bei umetokana na ukosefu wa chakula kutoka nchi jirani hali inayochangia kuwepo kwa uhaba wa chakula kwa baadhi ya maeneo.

Rais Magufuli amekuwa akipinga kuwepo kwa tatizo la chakula huku viongozi wa dini wakiagiza waumini wao kufanya maombi ya mvua kutokana na upungufu wa chakula na baa la njaa kwa baadhi ya maeneo nchini.

Taasisi ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) tayari zimetoa msimamo wake kutokana na nja nchini.

Miongoni mwa wanasiasa wanaoitahadharisha serikali kutokana na upungufu wa chakula nchini ni pamoja na Edward Lowassa aliyeshauri serikali kaungalia msimamo wake kuhusu chakula nchini.

Lowassa, aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema mwaka 2015 aliitaka serikali kuwa na tahadhari na kueleza kuwa, yeye na chama chake wamejadili namna ya kuangalia uwezekano wa kupata chakula na kuwapa Watanzania.

Rais Magufuli alipokuwa mjini Bariadi mkoani Simiyu alisema, suala la kuwepo kwa njaa ni uzushi.

“Wapo wafanyabiashara wengine wachache waliokuwa wamezoea panapotokea matatizo kidogo tu ya ukame wanatumia vyombo vya habari ikiwa pamoja na magazeti wanayoyaamini wao sio magazeti yote, pamoja na baadhi ya wanasiasa kuzungumza Tanzania kuna njaa.

“Anayejua njaa ni Rais na sio gazeti fulani mimi ndiyo niliyepewa dhamana ya kuwaongoza Watanzania,” alisema.

Wakati Waziri Majaliwa akiagiza tani milioni 1.5 ziingizwe sokono kwa ajili ya kukabiliana na makali ya bei ya vyakula kupanda, Rais Magufuli amekuwa akinukuliwa akisema serikali haina shamba hivyo haiwezi kutoa chakula kwa wananchi.

Taarifa hiyo iliibua mijadala kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi ya wachangiaji wakihoji serikali zilizopita ziliwezaje kukabiliana na tatizo la njaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Nchimbi aanika ugonjwa wa CCM

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emanuel Nchimbi,...

Habari za Siasa

Chadema yapuliza kipyenga uchaguzi viongozi kanda

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeanza maandalizi ya uchaguzi...

Habari za Siasa

CCM :Hatutaki ushindi wa makandokando uchaguzi Serikali za mitaa

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakihitaji ushindi wa makandokando katika...

Habari za Siasa

Makala: Puuzeni wanasiasa wanaojigamba wanaweza kubadili maamuzi ya mahakama

Spread the loveKATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...

error: Content is protected !!