Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Z’bar ‘mikononi’ mwa Lowassa, Maalim Seif
Makala & UchambuziTangulizi

Z’bar ‘mikononi’ mwa Lowassa, Maalim Seif

Edward Lowassa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema (kulia) akiteta jambo na Maalim Seif Sharrif Hamad, Katibu Mkuu wa CUF
Spread the love

UMOJA wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ukiongozwa na Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu wa CUF na Edward Lowassa, Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema wanatarajiwa kuunguruma leo visiwani Zanzibar, anaandika Charles William.

Viongozi hao watawasha moto katika Skuli ya Fuoni, Zanzibar katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani.

Lowassa ambaye alikuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema, katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 anashiriki uzinduzi wa kampeni hizo sambamba na Maalim ambaye pia alikuwa mgombea Urais Visiwani Zanizbar kupitia CUF.

Wakati Lowassa na Maalim Seif wakizindua kampeni hizo leo, vigogo wengine kutoka vyama washirika wa Ukawa wanatarajia kupanda jukwaa katika siku zingine za kampeni ikiwemo Januari 21 mwaka huu ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kampeni.

Tayari Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimezindua kampeni yake siku nne zilizopita ambapo Abdurahman Kinana, Katibu Mkuu wa chama hicho akiambatana na viongozi wengine wa chama hicho na jumuiya zake walihutubia.

Miongoni mwa waliohudhuria uzinduzi wa CCM ni Shaka Hamdu, Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM).

Kwa mujibu wa Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema – Zanzibar viongozi mbalimbali wa Chadema taifa akiwemo Mwenyekiti, Freeman Mbowe na Tundu Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, watashiriki kampeni za Dimani kwa nyakati tofauti.

Salim Bimani, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma wa CUF amenukuliwa akisema “Patakuwa hapatoshi hapa Skuli ya Fuoni, Lowassa anakubalika sana hapa na pia atapata nafasi ya kuwashukuru Wazanzibar kwa kura nyingi walizompigia katika uchaguzi wa 2015.”

Mbali na viongozi wa Chadema kuwa katika ratiba ya kushiriki uchaguzi mdogo wa Dimani pia inatarajiwa kuwa James Mbatia, Mbunge wa Jimbo la Vunjo na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi anatarajiwa kutua Visiwani Zanzibar pia.

Itakumbukwa kuwa uchaguzi huo mdogo utafanyika tarehe 22 Januari, 2017 kufuatia kufariki dunia kwa Hafidh Ally Tahir aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kabla ya kufariki dunia 11 Novemba, 2016 mkoani Dodoma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Je, miji ya Uingereza inafilisika?

Spread the loveMNAMO 1890, mwandishi mmoja wa habari Mmarekani aitwaye Julian Ralph...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

error: Content is protected !!