August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kubenea ajitosa ubunge Unguja

Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo, akizungumza na wapiga kura wake

Spread the love

MBUNGE wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea, leo Jumapili, ataungana na viongozi

waandamizi wa upinzani nchini, Edward Lowassa na Maalim Seif Sharif Hamad, kumpigia kampeni mgombea ubunge jimbo la Dimani, Unguja, anaandika Mwandishi Wetu.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Kubenea alisema, “ninakwenda Unguja kutafuta mbunge. Nakwenda kuongeza nguvu. Nakwenda Unguja, kushinda.”

Kubenea, mmoja wa wabunge machachari wa upinzani nchini anasema, ameamua kwenda Unguja ili kusaidia harakati za ukombozi kwa kuhakikisha Chama cha Wananchi (CUF), kinashinda katika uchaguzi huo.

Uchaguzi mdogo wa Dimani Unguja, unafanyika kufuatia aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Hafidhi Aly Twahir, kufariki dunia mwishoni mwa mwaka jana mjini Dodoma. Habari zaidi juu ya mkutano wa kampeni katika jimbo la Dimani, usikose kusoma MwanaHALISI Online – Mhariri.

error: Content is protected !!