September 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

803 wafariki, 33,789 wakiambukizwa Uviko-19 Tanzania

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu

Spread the love

 

SERIKALI imesema jumla ya watu 803 wamepoteza maisha kwa ugonjwa wa korona huku 33,789 wakiambukizwa tangu kuripotiwa kwa kisa cha kwanza nchini. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo tarehe 16 Machi 2022 jijini Dodoma na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, wakati akitoa tamko la hali ya Uviko-19 ikiwa ni miaka miwili tangu kuripotiowa kwa kisa cha kwanza nchini.

Amesema kuwa Katika kipindi chote Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, mashirika yasiyo ya kiserikali, Taasisi za Dini na wanataaluma wa afya na wananchi kwa ujumla imeendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kukabiliana na ugonjwa huu.

Aidha amesema kuwa katika kipindi hicho serikali imeweza kuongeza wigo wa uchunguzi wa kimaabara wa UVIKO-19 ambapo kwa sasa kuna maabara saba ndani ya nchi zenye uwezo wa kupima UVIKO19 ukilinganishab na Maabara moja ya Afya ya Jamii iliyokuwepo wakati wa kulipuka kwa ugonjwa huo mwezi Machi 2020.

“Maabara hizi ni pamoja na Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, Maabara katika Hospitali za Kanda za Bugando, Mbeya na Maabara katika Hospitali za Rufaa za Mikoa ya Dodoma, Arusha, Kigoma, na Maabara iliyopo katika Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.

“Aidha, Serikali imesimika mitambo 15 ya hewa tiba ya Oksijeni katika Hospitali mbalimbali nchini ili kuweza kutoa huduma za wagonjwa mahututi wanaohitaji uangalizi maalum.

“Serikali pia imeendelea kuikinga jamii kwa kuwezesha upatikanaji wa chanjo ya UVIKO-19 nchini, ambapo hadi kufikia tarehe 12 Machi 2022, jumla ya watu 2,820,545 wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, wamepata chanjo kamili dhidi ya ugonjwa huu.

“Idadi hii ni sawa na asilimia 9.17 ya watanzania 30,740,928 wenye umri wa miaka 18 na kuendelea ambao wanakidhi vigezo vya kuchanja.

“Idadi hii bado hairidhishi kwa kuwa ili tuweze kufikia kinga ya jamii (Heard immunity) tunapaswa kuchanja angalau asilimia 70 ya watu wenye umrii wa miaka 18 na kuendelea.

“Hali ya kiwanjo cha uchanjaji Kimikoa ni kama ifuatavyo,Ruvuma asilimia 23, Katavi asilimia 14, Dodoma asilimia 13, Mtwara asilimia 12, Mara asilimia 11, Mwanza asilimia 11, Lindi asilimia 10, Dar-es-Salaam asilimia 10, Simiyu asilimia 10, Pwani asilimia 9, Kilimanjaro asilimia 9, Kagera asilimia 9 na Mbeya asilimia 9” amesema Ummy.

Mikoa mingine ameitaja kuwa ni Arusha asilimia 8,Geita asilimia 7, Shinyanga asilimia 7, Iringa asilimia 7, Njombe asilimia 7 Rukwa asilimia 6, Morogoro asilimia, 6 Tanga asilimia 5, Kigoma asilimia 5, Tabora asilimia 5, Singida asilimia 5, Songwe asilimian 4 na Manyara asilimia 3.

Amesema kwa Kuzingatia hali hiyo , Mikoa inahitaji kuongeza juhudi katika kuhimiza wananchi kujitokeza kuchanja.

Hata hivyo amesema kuwa hali ya UVIKO-19 katika wimbi la nne nchini kwa sasa imepungua kwa kiasi kikubwa tokea lilipoanza mwanzoni mwa mwezi Desemba 2021 ambapo kwa mwezi Desemba 2021 jumla ya watu 4,285 walithibitika kuwa na maambuzi ya ugonjwa huu.

Amesema Kwa upande wa mwezi Januari 2022 wagonjwa waliothibitika walikuwa 2,737 na kwa kipindi cha mwezi Februari 2022, jumla ya wagonjwa 401 walithibitika kupata maambukizi ya ugonjwa huu.

Amesena kwamba Kupungua kwa maambukizi mapya ya ugonjwa wa COVID-19 kumeripotiwa pia katika baadhi ya nchi Duniani huku kukiambatana na kulegezwa kwa masharti ya kuzuia kusambaa kwa maambukizi.

error: Content is protected !!