Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Manyara, Songwe zashika mkia chanjo Uviko-19
Afya

Manyara, Songwe zashika mkia chanjo Uviko-19

Spread the love

 

MKOA wa Manyara umeshika nafasi ya mwisho kwa uchanjaji wa UVIKO-19 ikiwa na asilimia tatu tu ya watu waliopata chanjo hadi sasa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Hayo yamebainisha leo jumatano tarehe 16 Machi 2022 na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wakati akitoa taarifa ya hali ya UVIKO- 19.

Mikoa mingine iliyofanya vibaya kwenye utoaji chanjo ni Songwe asilimia nne,Tanga, Kigoma, Tabora, Singida asilimia tano.

Mingine ni Morogoro na Rukwa asilimia sita; Geita, Shinyanga, Iringa na Njombe asilimia saba; Arusha asilimia nane; Pwani, Kilimanjaro, Kagera na Mbeya asilimia tisa.

Mkoa uliongoza ni Ruvuma asilimia 23, ukifuatiwa na Katavi asilimia 14, Dodoma asilimia 13, Mtwara asilimia 12, Mara asilimia 11, Mwanza asilimia 11 na Lindi, Dar-es-Salaam na Simiyu zikiwa na asilimia 10.

Mwalimu amesema hadi kufikia tarehe 12 Machi 2022, jumla ya watu 2,820,545 wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, wamepata chanjo kamili dhidi ya ugonjwa huu.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu

“Idadi hii ni sawa na asilimia 9.17 ya watanzania 30,740,928 wenye umri wa miaka 18 na kuendelea ambao wanakidhi vigezo vya kuchanja.

“Idadi hii bado hairidhishi kwa kuwa ili tuweze kufikia kinga ya jamii (Heard immunity) tunapaswa kuchanja angalau asilimia 70 ya watu wenye umrii wa miaka 18 na kuendelea.

Amesema kwa Kuzingatia hali hiyo , Mikoa inahitaji kuongeza juhudi katika kuhimiza wananchi kujitokeza kuchanja.

Hata hivyo amesema kuwa hali ya UVIKO-19 katika wimbi la nne nchini kwa sasa imepungua kwa kiasi kikubwa tokea lilipoanza mwanzoni mwa mwezi Desemba 2021 ambapo kwa mwezi Desemba 2021 jumla ya watu 4,285 walithibitika kuwa na maambuzi ya ugonjwa huu.

Amesema Kwa upande wa mwezi Januari 2022 wagonjwa waliothibitika walikuwa 2,737 na kwa kipindi cha mwezi Februari 2022, jumla ya wagonjwa 401 walithibitika kupata maambukizi ya ugonjwa huu.

Amesena kwamba Kupungua kwa maambukizi mapya ya ugonjwa wa COVID-19 kumeripotiwa pia katika baadhi ya nchi Duniani huku kukiambatana na kulegezwa kwa masharti ya kuzuia kusambaa kwa maambukizi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

error: Content is protected !!