Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa 2000 wahofiwa kufariki kwa kimbunga Daniel
Kimataifa

2000 wahofiwa kufariki kwa kimbunga Daniel

Spread the love

ZAIDI ya watu 2000 wahofiwa kupoteza maisha huku maelfu wakiwa hawajulikani walipo baada ya kimbunga Daniel kuikumba nchi ya Libya. Anaripoti isaya Temu, TUDARCo…(endelea).

Waziri Mkuu wa Mashariki Osama Hamad amethibitisha kutokea kwa janga hilo lililoanza wiki iliyopita na kuomba msaada wa kimataifa kusaidia uokoaji.

Amesema mfumo wa hali mbaya ya hewa, uliopewa jina la kimbunga Daniel, umeleta mvua kubwa ya kihistoria katika bahari ya Mediterania na Afrika Kaskazini katika kipindi cha wiki moja iliyopita.

Amesema dhoruba hiyo ya bahari imeleta maafa makubwa ya mafuriko na kusababisha kuzama kwa maeneo ya mitaa baada ya kuiathiri zaidi eneo la mashariki ya Libya, Uturuki na Bulgaria.

Amesema tangu kuanguka kwa utawala wa Muammar Gaddafi, 2014 Libya imegawanyika katika Serikali mbili zenye ukinzani ambapo serikali zote zilitangaza siku tatu za maombolezo baada ya maafa ya kimbunga Daniel.

Waziri Mkuu katika Mji wa Tripoli, Abdulhamid Dbeiba siku ya Jumapili alitangaza hali ya hatari, akitaka bendera zipeperushwe nusu mlingoti huku pia akiagiza mashirika yote ya serikali kushughulikia mara moja uharibifu wa kimbunga hicho.

“Hali ni mbaya,” amesema Essam Abu Zeriba, Waziri wa mambo ya ndani wa serikali ya Mashariki mwa Libya.

Msemaji wa Jeshi linalodhibiti Mashariki mwa Libya, Ahmed Mismari ametangaza kuwa Derna ni eneo lililokumbwa na maafa makubwa baada ya mabwawa makubwa mawili ya maji yamepasuka na kufagia vitongoji na mitaa ya eneo hilo kuelekea baharini huku akisema kati ya watu 5,000 hadi 6,000 wamepotea.

“Baada ya mabwawa mawili kuvunjika kutokana na msukumo wa maji, matokeo yake madaraja matatu yaliharibiwa. Maji yanayotiririka yaliielekea kwenye mitaa yote na hatimaye kuitupa baharini,” ameeleza Mismari.

Georgette Gagnon, Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Kibinadamu nchini Libya, amesema ripoti za awali zinaonyesha kwamba vijiji na miji kadhaa zimeathirika sana na mafuriko makubwa, uharibifu wa miundombinu, na upotevu wa Maisha.

Serikali za nchi mbalimbali duniani zimeonesha kuguswa na maafa hayo nchini Libya na kutuma salamu za rambirambi, misaada ya kibinadamu na timu za uokoaji kusaidia ikiwemo Misri, Rais wa Falme za Kiarabu, Algeria, na Qatar.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!