Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Askofu Bagonza ampa mbinu Samia jina liandikwe kwa wino wa dhahabu
Habari za SiasaTangulizi

Askofu Bagonza ampa mbinu Samia jina liandikwe kwa wino wa dhahabu

Rais Samia akisalimiana na Askofu Bagonza
Spread the love

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Karagwe, Dk. Benson Bagonza amemtaka Rais Samia kuweka mfumo mzuri wa kidemokrasia nchini ili jina lake liandikwe kwa wino wa dhahabu. Anaripoti Isaya Temu, TUDARCo…(endelea).

Ameyasema hayo leo tarehe 12 Septemba 2023 katika mkutano maalum wa Vyama vya Siasa na Wadau wa Demokrasia unaofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam wakati akiwasilisha hoja zake.

Amesema kwa kuwa marais wengine waliopita wameshafanya mambo makubwa katika uongozi wao, basi yeye aweke mfumo mzuri wa kidemokrasia ili jina lake liandikwe na lisisahaulike.

“Ningependa kwa moyo mweupe pia niseme Marais waliopita wote wamefanya vitu vingi, madaraja wamejenga, barabara wamejenga, majengo wamejenga lakini kuna kitu kimoja ambacho Mheshimiwa Rais inabidi akifanye ili jina lake liandikwe kwa wino wa dhahabu.

“Kama Mheshimiwa Kikwete alivyowaambia akina Mzee Warioba, alisema majina yao yataandikwa kwa wino wa dhahabu, sasa Mheshimiwa Rais akituwekea mfumo mzuri wa kidemokrasia hatutamsahau katika maisha yake yote,” amesema Askafu Bagonza.

Pia Askofu Bagonza ameeleza kuwa kwa upande wake anaona kuna mgongano baridi kati ya kikosi kasi na kazi iliyofanywa na Tume ya Mzee Warioba huku akishauri kuwa kunahitajika kuunganisha kazi hizo ziwe moja ili taifa liweze kusonga mbele na kutoka kwenye hali ya Mkwamo iliyopo ya kupatikana kwa katiba mpya.

Pamoja na maoni hayo, Askofu Bagonza ametoa pongezi kwa uamuzi wa serikali kutaka kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali ikiwemo sheria za uchaguzi na vyama vya siasa huku akishauri maboresho ya sheria hizo yafanyike kwa uwazi

“Serikali imeshatoa tangazo la kwamba Oktoba mwaka huu wanapeleka marekebisho au maboresho ya sheria, ningependa kusema kwa moyo safi kuwa, kwamba kwa uzoefu tulikotoa kutegemea uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ujao ufanyike bila marekebisho yoyote tutakuwa tunajidanganya.

“Kwa hiyo napenda kushukuru hiyo dhamira na nihimize maboresho hayo yafanyike kwa njia ya uwazi ili tuondokane na mshangao, yaani aliyeshinda anashangaa na aliyeshindwa anashangaa, waliosimamia wanashangaa. Nafikiri tunatakiwa kuondokana na hali hiyo,” ameongeza Askofu Bagonza.

1 Comment

  • Ask Bagonza
    Umezungumza vema katika hotuba yako Kama kawaida yako na hali hii inanipa moyo kwamba bado tunao viongozi wa dini wanaopenda nchi na watu wake kwa moyo wa dhati. Nami nasema kwa yote uliochangia nawe jina lako linastahili kuandikwa kwa wino wa dhahabu. Tutaendelea kukumbuka katika HISTORIA ya nchi hii. Kukukosa katika uongozi wa juu KKKT ilikuwa ni bahati mbaya. There is still another day. Stay blessed

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the loveCHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!