March 9, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Mkuu Uswatini afariki dunia

Cyril Ramaphosa, Rais wa Afrika Kusini

Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Uswatini, Ambrose Dlamini, amefariki dunia jana Jumapili tarehe 13 Desemba 2020, hospitalini nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa iliyotolewa jana Jumapili na Naibu Waziri Mkuu wa Uswatini, Themba Masuku ilieleza, Dlamini mwenye miaka 52, alifikwa na mauti wakati akiendelea na matibabu.

Katika taarifa hiyo, Masuku hakueleza chanzo cha kifo cha Dlamini, aliyekuwa waziri mkuu kuanzia 27 Oktoba 2018.

Hata hivyo, hivi karibuni, waziri mkuu huyo, alipimwa na kukutwa na maambukizo ya virusi vya corona (COVID-19).

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ametuma salamu za rambirambi kwa familia, marafiki na wananchi wa Uswatini kutokana na kumpoteza kiongozi wao na kuwataka kuwa watulivu katika kipindi hiki cha maombolezo.

error: Content is protected !!