Tuesday , 16 April 2024
Home Kitengo Michezo Liverpool wapewa mfupa uliowashinda Manchester United
Michezo

Liverpool wapewa mfupa uliowashinda Manchester United

Spread the love

DROO ya michuano ya Klabu Bingwa Ulaya (Uefa) imechezeshwa hii leo ambapo klabu ya Liverpool itawavaa vigogo wa Ujerumani RB Leipzing ambao waliwaondosha Manchester United kwenye hatua ya makundi mara baada ya kupata ushindi wa mabao 3-2. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam …  (endelea).

RB Leipzing ambao walishika nafasi ya pili kwenye kundi H, wakiwa na pointi 12 watacheza mchezo wa kwanza dhidi ya Liverpool wakiwa nyumbani kwenye dimba la Red Bull Arena nchini Ujerumani.

Liverpool ambao wamevuka hatua hiyo mara baada ya kuwa vinara kwenye kundi D, mbele ya Atalanta, Ajax na Midtyjland.

Michezo mingine kwenye kundi hiyo itawakutanisha Barcelona dhidi ya PSG, Lazio kuwakabili Bayern Munchen, Porto dhidi ya Juventus, Sevilla kuwakabili Dortumund, Atalanda itawakaribisha Real Madrid, huku Atletico Madrid watawavaa Chelsea kwenye mchezo wa kwanza.

Fainali za michuano hiyo zinatarajiwa kuchezwa mwakani kwenye jiji la Instabul, Uturuki huku mabingwa watetezi wakiwa ni Bayern Munchen.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

Michezo

TFF, Amrouche ngoma nzito

Spread the loveVIPENGELE vya mkataba wa kazi aliotia saini Kocha Mkuu wa...

Michezo

Jumapili ya maokoto na Meridianbet ni hii

Spread the love BAADA ya jana kushuhudia mitanange kibao kutoka ligi mbalimbali,...

error: Content is protected !!