Saturday , 11 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Siku za Makonda zinahesabika?
Habari za Siasa

Siku za Makonda zinahesabika?

Paul Makonda, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Spread the love
MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Albert Makonda na mkewe, Mary Felix Massenge, wamepigwa marufuku kuingia nchini Marekani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa iliyotolewa na wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani jana Ijumaa, tarehe 31 Januari 2020,  imeeleza kuwa kuzuiwa kwa Makonda kuingia nchini humo, kunatokana na kile kinachoitwa, “ushiriki wake katika ukandamizaji wa haki za binaadamu.”

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Michael Pompeo ameeleza katika mtandao wake wa Twitter, kwamba serikali mjini Washington, ina taarifa za uhakika kuwa Makonda amehusika katika uvunjifu wa haki za binadamu kupitia nafasi yake kama mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.

Katika nafasi yake hiyo, pia amelaumiwa kwa kukandamiza upinzani wa kisiasa, kukandamiza haki ya kujieleza, na kushambulia makundi yasiyo na sauti,” ameeleza kachero huyo wa zamani wa CIAA.

Makossa mengine anayoshutumiwa Makonda, ni pamoja na kunyima watu haki ya kuishi, haki ya uhuru wa kujiamulia mambo na usalama wa watu.

Amesema, “Paul Christian Makonda hataruhusiwa kuingia Marekani kwa kushiriki kwake katika ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu. Tuna wasiwasi mkubwa juu ya kuporomoka kwa heshima ya haki za binadamu na utawala wa sheria nchini Tanzania.

Hatua ya Marekani kumpiga marufuku Makonda kuingia nchini humo, kunaweza kuwa mwazo wa safari ya mwanasiasa huyo, kufikishwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu dhidi ya mwanadamu ya The Hugue, iliyopo nchini Uholanzi.

Taarifa hiyo ya serikali ya Marekani pia imeikosoa Tanzania juu ya hali ya haki za binaadamu; hali hiyo inajumuisha matendo ya viongozi yanayokandamiza uhuru wa kujieleza, uhuru wa jumuiya, uhuru wa kukusanyika kwa amani, kukandamiza makundi yasiyo na sauti na upinzani wa kisiasa na kutishia maisha.

“Hatua hizi dhidi ya Paul Christian Makonda zinatilia mkazo hofu yetu ya kuvunjwa kwa haki za binadamu Tanzania pamoja na kuunga mkono kwetu uwajibikaji kwa wale wote wanaohusika katika ukandamizaji huo. Tunaitaka serikali ya Tanzania kuheshimu haki za binadamu na za msingi kama uhuru wa kujieleza, jumuiya na mikusanyiko ya amani,” imeeleza taarifa hiyo.

Wakati Marekani ikimpiga marufuku kuingia nchini humo, shirika la kutetea haki za binadamu nchini Tanzania – Legal and Human Rights Center (LHRC) – kimeondoa kwenye tovuti yake, taarifa inayomuonyesha mkuu huyo wa mkoa akitelembelea mabanda yake, leo tarehe 1 Februari 2020.

Kwa mujibu wa kituo hicho, Makonda alifika kwenye banda lao wakati akizindua wiki ya sheria nchini na kupata fursa ya kuzungumza na baadhi ya maofisa wao na kupiga nao picha ambazo zilisambazwa kwenye mtandao wao.

Hata hivyo, mara baada ya tukio hilo, wananchi mbalimbali, wakiwamo wanaharakati wa utetezi wa haki ya kuishi, haki ya kutoa maoni na haki nyingine za binadamu, wamekituhumu kituo hicho kwa uamuzi wake huo na kudai kuwa kitendo hicho, ni sawa na kubariki matendo yake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Vijana UVCCM Kagera wataka mwenyekiti wao ajiuzulu

Spread the loveVIJANA wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera wamemtaka Mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina awavaa mawaziri wanaompelekea majungu Rais Samia

Spread the loveMBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM) amewataka baadhi ya mawaziri...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

THRDC, Wizara ya Katiba wajadili uanzishaji haki binadamu katika biashara

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), umefanya...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Sitta ang’ang’ana wanafunzi watibiwe bure, Serikali yagoma

Spread the loveMBUNGE wa Urambo, Margaret Sitta, ameishauri Serikali iweke utaratibu wanafunzi...

error: Content is protected !!