December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mchungaji Mwamposa atuhumiwa kwa mauti, atiwa mbaroni Dar

Spread the love

MCHUNGAJI na Mtume Boniface Mwamposa, kiongozi wa Kanisa la Inuka Uangaze, amekamatwa na polisi Jijini Dar es Saalam, baada ya kusababisha vifo vya watu 20 na majeruhi 16, mjiji Moshi jana. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amesema kuwa kiongozi huyo wa kiroho alikimbia kutoka Moshi na kukamatiwa Dar es saalam na tayari ameshasafirishwa kurudishwa Moshi na taratibu za upelelezi zinaendelea.

Simbachawene, leo tarehe 2 Februari 2020, amesema kwa sasa kiongozi huyo wa kidini anashikiliwa na polisi.

Amesema, baada ya tukio kutokea vifo, walienda uwanja wa ndege kutokana na taarifa kuwa, angesafiri kwa ndege lakini haikuwa hivyo na badala yake aliamua kusafiri kwa gari kwenda Dar es Salaam.

Wakati Mwamposa wa Kanisa la Inuka Uinuliwe akishikiliwa na polisi, jeshi hilo mkoani Kilimanjaro, linawashikilia watu kadhaa akiwemo Elia Mwambapa, Mchungaji wa Kanisa la Calvary Assemblies of God.

Tukio hilo lilitokea usiku wa Februari Mosi, 2020 . Taarifa zaidi zinaeleza, mafuta hayo yanayoelezwa kuwa ya upako, yalimwagwa kwenye milango ya kutokea ya kanisa hilo hiyo, waumini waligombania kukanyaga wakati wakitoka na kusababisha mkanyakago uliopelekea vifo hivyo.

Awali, jeshi hilo mkoani Kilimanjaro, linamtaka Mwamposa kujisalimisha mwenyewe, kutokana na kuhusishwa na vifo hivyo wakati waumini hao waliposhiriki kwenye kongamano katika Uwanja wa Majengo.

Kibali cha kingamano hilo la siku tatu, kiliombwa na Mchungaji Mwambapa na kwamba, mchungaji huyo aliomba mafuta hayo kutoka kwa Mwamposa.

“Ni kweli, tunamtafuta Mwamposa ambaye pia anajulikana kwa jina la Bulldozer kwa mahojiano,” alisema Salum Hamduni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro. Amesema, taarifa za vifo mpaka sasa ni watu 20, na kwamba wanawake 15, mwanaume mmoja na watotot wadogo wane (wakiume wawili na wakike wawili).

Hata hivyo, leo tarehe 2 Februari 2020, alilazimika kufupisha ibaya yake jijini Dar es Salaam na kuwaeleza waumini kwamba, anaelekeo Moshi kuitikia wito wa polisi ndio akakamatwa.

error: Content is protected !!