Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais mpya Malawi ateua maswahiba zake
Kimataifa

Rais mpya Malawi ateua maswahiba zake

Lazarus Chakwera, Rais wa Malawi
Spread the love

RAIS mpya wa Malawi, Lazarus Chakwera ameanza uteuzi wa watu watakaomsaidia kuendesha serikali yake wakiwemo maswahiba zake. Inaripoti itandao ya kimataifa … (endelea).

Rais huyo aliyetokana na chama cha upinzani cha DPP, ameanza kuongoza taifa hilo baada ya kuapishwa juzi Jumapili tarehe 28 Juni 2020.

Tarehe 27 Juni 2020, Tume ya Uchaguzi ya Malawi (MEC) ilimtangaza Chakwera kushinda kwa asilimia 58.57 na kumwangusha Peter Mutharika, aliyekuwa akitetea kiti hicho.

Kwenye uteuzi wake alioufanya baada ya kuapishwa, amemteua Saulos Chilima, ambaye alikuwa naye bega kwa beka katika harakati zake za kuapishwa kuwa Waziri wa Uchumi, Mipango na Maendeleo.

Chilima ambaye pia ni Makamu wa Rais anatajwa kuwa miongoni mwa watu muhimu ‘waliocheza karata’ kuhakikisha uchaguzi wa rais unarudiwa baada ya kuonekana kuna dosari.

Ni miongoni mwa swahiba wa karibu wa Chakwera ambaye kwa pamoja awali waliunda umoja uliojulikana kwa jina la Tonse Alliancedhidi ya Mutharika.

Felix Mlusu ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha. Awali, alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Nico Holdings Plc, taasisi ya fedha yenye matawi yake Malawi, Tanzania, Uganda, Zambia na Msumbiji.

Modecai Msiska, ambaye ni mwanasheria wake kwenye kesi ya kupinga matokeo na mtu wa karibu, ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Chikosa Silungwe, ambaye ni mwanasheria wake mwingine kwenye kesi yake ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa awali, amemteua kuwa Mwanasheria Mkuu (AG).

Kabla ya uteuzi huo, Silungwe alikuwa akihudumu kwenye Ofisi ya Tume ya Sheria ya Malawi.

Richard Banda ameteuliwa kuwa Waziri wa Usalama wa Ndani.

Uchaguzi huo umefanyika tarehe 23 Juni 2020 baada ya ule wa awali, uliofanyika Mei 2019 kufutwa na mahakama nchini humo Februari 2020 kutokana na kubainika ulitawaliwa na dosari.

Katika uchaguzi huo wa Mei 2019, Rais Mutharika aliibuka mshindi kwa kupata asilimia 38.57 huku Chakwera akipata asilimia 35.41.

Hata hivyo, Chakwera hakukubali matokeo hayo na kuamua kufungua kesi mahakamani kuyapinga na Februari 2020, akashinda kesi hiyo na uchaguzi ukarudiwa na yeye kuibuka mshindi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!