MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli amerejesha fomu za kuwania urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Rais Magufuli amerejesha fomu hizo leo Jumanne tarehe 30 Juni 2020 makao makuu ya CCM, Dodoma na kupokelewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Bashiru Ally.
Hafla hiyo fupi imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM, Serikali na wanachama wa chama hicho wakiwemo wenyeviti wa chama hicho nzima waliowasilisha kila mmoja fomu za udhamini.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa, Dk. Bashiru amesema, jumla ya wanachama zaidi ya milioni 1 waliojitokeza kumdhamini kutoka mikoa 32 na jumuiya zake tatu za wazazi, vijana na wanawake.
Dk. Bashiru amesema, “fomu nimezipokea na nimedhibitisha kuwa amezijaza vizuri.”
Amesema, leo Jumanne saa 10 jioni ndiyo siku ya mwisho ya uchukuaji na urejeshaji fomu za urais ndani ya chama hicho. Aliyechukua ni mmoja tu ambaye ni Rais Magufuli.

Mchanganuo wa wadhamini kila mkoa
- Arusha – 22,706
- Dar es Salaam -71,491
- Geita – 89,595
- Iringa – 12,542
- Kagera – 27,245
- Katavi – 5,071
- Kaskazini Pemba –2,575
- Kaskazini Unguja – 1,141
- Kigoma – 30,220
- Kilimanjaro – 23,434
- Singida – 13,452
- Kusini Pemba – 350
- Lindi – 9,515
- Magharibi Z’bar – 1,005
- Manyara –19,972
- Mara – 87, 550
- Mbeya – 11,600
- Mjini Z’bar – 2,394
- Morogoro –117,450
- Mtwara – 7,566
- Njombe – 17,810
- Pwani – 20,603
- Rukwa – 5,600
- Ruvuma – 56, 350
- Shinyanga – 12,000
- Simiyu – 3,693
- Songwe – 11,744
- Tabora – 29,489
- Tanga – 62,839
- Mwanza –
- Kusini Unguja –
32.Dodoma – 44, 415
Jumuiya za chama
- UWT – 66,633
- Wazazi – 48,329
- UVCCM – 100,360
Leave a comment