January 22, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mtu mweusi afanyiwa unyama Marekani

Spread the love

GEORGE Floyd (46), raia mweusi wa Marekani, ameuawa kwa kukandamizwa shingo na polisi mzungu wa Jiji la Minnesota, polisi wanne wamefukuzwa kazi kutokana na mkasa huo. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Katika video iliyorekodiwa wakati akifanyiwa unyama huo, Floyd alilalamika kukandamizwa kwenye shingo huku akisisitiza anakosa hewa, hakusikilizwa na hata alipopelekwa hospitali, hakuwezi kupona.

Taarifa zaidi zinaeleza, Floyd alikuwa akifanya kazi kama ofisa wa usalama kwenye mgahawa mmoja jijini humo.

Floyd alikabiliana na mteja mmoja aliyefika mgahawani hapo akijaribu kununua bidhaa kwa kutumia noti bandia ya Dola 20.

Alipoanza kumkabili, ndipo mvutano ukatokea na katika dakika chache polisi walipofika hapo, kulikuwa na kutoelewana kati ya polisi hao na Floyd.

Kutokana na mvutano huo, polisi walimweka chini, walimfunga pingu na kuanza kumkandamiza kwa goti juu ya shingo yake. Wakati akikandamizwa, Floyd alisikika akisema ‘msiniue.’

Polisi mmoja alisikika akimwambia mwenzake aondoe goti lake juu ya shingo ya Floyd, kwa maelezo alikuwa ametulia na hakukuwa na haja ya kutumia nguvu. Hakusikilizwa.

Mwingine alimwambia mwenzake ‘pua yake inatoa damu, ondoa goti. Ondoka kwenye shingo yake.” Na hata alipotoa, Floyd alikuwa tayari ameishiwa nguvu ambapo alipakizwa kwenye gari la wagonjwa na kupelekwa hospitali.

Medaria Arradondo, Ofisa Mkuu wa Jeshi la Polisi Minnesota amesema, licha ya Floyd kudhaniwa kutenda kosa, bado alikuwa na haki ya kusikilizwa na kuishi “kwa polisi hao wanne sasa sio wafanyakazi wetu.”

Jacob Frey, Meya wa Minnesota amesema, hatua ya kwanza kutokana na unyama huo iliyotekelezwa ni kuwafukuza kazi polisi hao huku uchunguzi ukiendelea.

“Huu ni unyama usiostahili mtu yeyote kufanyiwa,” amesema Frey na kuongeza, “ninaamini kwamba kile nilichokiona ni kitendo cha makosa kwa kiwango chochote kile.”

Hata hivyo, taarifa zaidi zinaeleza Floyd hakuwa na silaha yoyote wakati wa mvutano huo. Shirika la Ujasusi la Marekani (FBI), limeeleza kuanza kuchunguza tukio hilo.

Kutokana na tukio hilo, jana Jumanne tarehe 26 Mei 2020, wananchi (weusi na weupe) wamekuwa wakiandamana kulaani kitendo alichofanyiwa Floyd, polisi wamekuwa wakitumia maji ya kuwasha kuwatawanya.

error: Content is protected !!