October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wagonjwa wa corona Z’bar wabaki 19, kidato cha sita kurejea Juni 1

Spread the love

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imetangaza kuregeza baadhi ya mambo wakati huu wa mapambano ya ugonjwa wa COVID-19 ikiwemo, kufungua shule kwa wanafunzi wa kidato cha sita tarehe 1 Juni, 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano tarehe 27 Mei, 2020 na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar imesema SMZ imechukua uamuzi huo ili kwenda sambamba na kilichofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Serikali ya Tanzania imetangaza kuvifungua vyuo vyote na wanafunzi wa kidato cha sita kuanzia tarehe 1 Juni, 2020 huku mitihani ya kidato cha sita ikianza tarehe 29 Juni hadi 16 Julai, 2020.

error: Content is protected !!