Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kikokotoo pasua kichwa kila kona
Habari MchanganyikoTangulizi

Kikokotoo pasua kichwa kila kona

Spread the love

CHAMA cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) wametoa tamko la kuunga mkono msimamo wa TUCTA kuhusu mkanganyiko Kikokotoo cha mafao ya pensheni yanayotolewa na mfuko wa hifadhi ya Jamii. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Mbali na kutoa tamko la kuunga mkono msimamo wa TUCTA, TALGWU wamepiga marufuku na kuwakemea baadhi ya watu ambao wamekuwa wakijitokeza kuwasemea wafanyakazi (Chama cha Waajiri) kwa madai kuwa wanakubaliana na kikokotoo hicho na kueleza kuwa wanaowasemea wafanyakazi wanyamaze kimya kwani hawajatumwa na wafanyakazi na hawana nia njema na wafanyakazi.

Akitoa tamko hilo Mwenyekiti wa TALGWU Taifa, Suleiman Kikingo alisema kuwa TALGWU haikubaliani kabisa na kanuni zinazomlipa mstaafu kiasi kidogo cha mafao ukilinganisha na kanuni zilizokuwepo awali.

Hata hivyo Mwenyekiti alisema kuwa ni kweli wajumbe na viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini walishiriki katika mchakato wa mafao mapya ya wastaafu lakini hawakukubaliana na serikali juu ya kikokotoo na mafao yanayopendekezwa na serikali ya kumlipa mstaafu kwa asilimia 25 kama fedha ya mkupuo.

Alisema kuwa jambo hilo halikuweza kufikia mwafaka kwani wajumbe na viongozi wa vyama vya wafanyakazi walitakaa hicho kikikotoo kwa maana kuwa kiwango hicho ni kidogo na kama wastaafu watapewa kiwango hicho cha fedha ni sawa na kutaka kuwaua mapema kwani kutokana na kuwepo kwa mishahara midogo na mafao ya mkupuo yatakuwa madogo.

“Ikumbukwe kwamba wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) ndiyo watumishi wa Umma wanaolipwa mishahara midogo na kuwa hali hiyo ndilo kundi linaloathirika na kanuni hii mpya kwa kumlipa mafao mstaafu ya mafao yake kwa asilimia 25 kama malipo ya mkupuo na kubakiza asilimia asilimia 75 ambazo serikali imepanga kuwalipa wastaafu kama pensheni ya kila mwezi,” alisema Kikingo.

Kutokana na hali hiyo TALGWU wamesema kuwa wanatoa wito kwa Waziri mwenye dhamana na Serikali kwa ujumla wake wakumbuke na kutambua mchango mkubwa wa wafanyakazi kwa nchi na walione jambo hilo katika mtazamo chanya.

“Kilio hiki cha wafanyakazi ambao ndio walipaji wakubwa wa kodi na wanaochangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi cha kupuuzwa.

“Tunaiomba seriali kurudi katika meza ya majadiliano na viongozi wa vyama vya wafanyakazi kwa lengo la kupata ufumbuzi wenye tija kwa maslahi ya wafanyakazi,” alisema Kikingo.

Kwa upande wake wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa TALGWU Taifa na mwakilishi wa wafanyakazi mkoa wa Kagera, Dk. David Mapuda alisema kuwa ni wakati wa serikali kukaa meza moja kumaliza mzozo huo na iwapo hawatakuwa tayari kufanya hivyo wafanyakazi ambao ni wapigakura wao watapewa mrejesho na kuona nini kifanyike.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

error: Content is protected !!