Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Lowassa, Sumaye, Maalim Seif, Zitto kumfuata Mbowe Kisutu kesho
Habari za SiasaTangulizi

Lowassa, Sumaye, Maalim Seif, Zitto kumfuata Mbowe Kisutu kesho

Spread the love

VIGOGO watatu wa kisiasa nchini, Edward Lowassa, Maalim Seif Sharif Hamad na Fredrick Suamye, kesho Ijumaa, wataongoza mamia ya wafuasi wa upinzani, kuelekea kwenye Mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam, kufuatilia kesi ya “kisiasa,” inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe. Anaripoti Saed Kubenea … (endelea).

Wengine watakaongozana na viongozi hao, ni Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) ambaye pia ni kiongozi mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, wabunge wa upinzani na baadhi ya viongozi wa vyama vingine.

Mbowe yuko kwenye mahabusu ya magareza ya Segerea, baada ya kufutiwa dhamana na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, tokea Novemba mwaka huu.

Mwingine ambaye yuko mahabusu ya Segerea baada ya kufutiwa dhamana na Mahakama ni mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.

“Kesho tarehe 21 Desemba 2018, saa mbili asubuhi, kwenye Mahakama ya Hakim Mkazi Kisutu, wafungwa wa kisiasa (Freeman Mbowe na Esther Matiko), wataletwa mahakamani kwa ajili ya kutajwa kesi yao, wakati wakisubiri kuitwa mahakama ya rufaa,” imeeleza taarifa ya viongozi hao.

Imesema, “Maalim Seif, Lowassa, Sumaye na Zitto, wamethibitisha kuongoza mamia ya wananchi kuhudhuria mahakamani. Shime kwa wapigania demokrasia, haki na utu, kujitokeza kwa wingi kuwalaki wafungwa hawa wa kisiasa.”

Washitakiwa wengine kwenye kesi hiyo, ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vicenti Mashinji; naibu katibu mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalimu na mbunge wa Kawe, Halima Mdee.

Wengine, ni Naibu katibu Mkuu Bara na mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Ester Bulaya, mbunge wa Bunda, Mchungaji Peter Msigwa, mbunge wa Iringa Mjini na John Heche, mbunge wa Tarime Vijijini.

Mbowe na wenzake, wanashitakiwa mahakamani kwa madai ya kuandamana bila kibali na kusababisha mauwaji ya mwanafunzi wa chuo cha usafirishaji cha taifa (NIT), Akwiline Akwilina.

Akwilina aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi, Februari mwaka huu, katika maeneo ya Mkwajuni jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo Polisi waliokuwa wakishikiliwa kwa tuhuma za mauaji hayo, waliachiwa huru kwa madai kuwa hakukuwa na ushahidi juu ya tuhuma hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the loveCHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!