Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Michezo Nyaraka kuamua hatma ya kesi ya Morison, Yanga
Michezo

Nyaraka kuamua hatma ya kesi ya Morison, Yanga

Bernard Morrison
Spread the love

KAMATI ya Sheria na hadhi ya Wachezaji inatarajia kutoa maamuzi juu ya kesi ya kimkataba kati ya mchezaji Benard Morrison na uongozi wa klabu ya Yanga, baada ya shauli hilo kusikilizwa kwa siku tatu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Elias Mwanjala jana Jumanne alieleza kuwa sakata hilo litatolewa maamuzi leo baada ya pande zote mbili kutakiwa kuwasilisha nyaraka ambazo ni muhimu na baadae kutoa hukumu.

“Kuna nyaraka moja ambayo haijakamilika na tunategemea kuipata kesho (leo) saa nne asubuhi tunaanza kikao na baadae kutoa uwamuzi, hapa tulipofika ni pazuri, msiwe na shaka muwe na subira,” alisema Mwanjala.

Mchezaji huyo ambaye Jumamosi alitambulishwa na klabu ya Simba licha ya klabu ya Yanga kudai kuwa Morrison bado anamkataba na klabu hiyo na kesi yao bado ipo kwenye Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya kamati ya Sheria.

Morrison alifika nchini 15 January, 2020 na kujiunga na klabu ya Yanga katika dirisha dogo la usajili kwa mkataba wa miezi sita, licha ya baadae Yanga kudai kuwa klabu hiyo ilimuongeza mkataba wa miaka miwili.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Piga pesa na mechi za UEFA

Spread the love  HATIMAYE leo hii ndio kitaeleweka nani aende Nusu Fainali...

Michezo

Idris Sultan anogesha msimu wa 3 wa Bridgerton

Spread the loveSTAA wa burudani kutoka ardhi ya Tanzania, Idris Sultan amenogesha...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya...

Michezo

Usiishie kuangalia tu game za leo, piga na mkwanja na Meridianbet

Spread the love  LIGI mbalimbali barani ulaya zitarejea tena Jumamosi ya leo...

error: Content is protected !!