Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu

Bosi ya Mikopo yafungua dirisha la rufaa

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo tarehe 21 Novemba 2018 imeanza kupokea rufaa za mikopo kwa mwaka wa masomo wa 2018/19 kwa njia ya mtandao. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na HESLB, inaeleza kuwa, dirisha la kuwasilisha rufaa hizo liko wazi kwa muda wa siku tano hadi Novemba 25 mwaka huu, ambapo wanafunzi wenye malalamiko wanatakiwa kutumia fursa hiyo.

“HESLB imefungua dirisha hili ili kutoa fursa kwa wanafunzi wahitaji ambao hadi sasa hawajapa mkopo au hawajaridhika na kiwango cha mkopo walichopangiwa, kuwasilisha maelezo na nyaraka kuthibitisha uhitaji wao,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, baada ya rufaa hizo kuwasilishwa na kupitiwa, wanafunzi watakaobainika kutimiza masharti na sifa watapangiwa mikopo kabla ya mwisho wa mwezi huu wa Novemba.

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo tarehe 21 Novemba 2018 imeanza kupokea rufaa za mikopo kwa mwaka wa masomo wa 2018/19 kwa njia ya mtandao. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea). Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na HESLB, inaeleza kuwa, dirisha la kuwasilisha rufaa hizo liko wazi kwa muda wa siku tano hadi Novemba 25 mwaka huu, ambapo wanafunzi wenye malalamiko wanatakiwa kutumia fursa hiyo. “HESLB imefungua dirisha hili ili kutoa fursa kwa wanafunzi wahitaji ambao hadi sasa hawajapa mkopo au hawajaridhika na kiwango cha mkopo walichopangiwa, kuwasilisha maelezo na nyaraka kuthibitisha uhitaji wao,” inaeleza…

Review Overview

User Rating: Be the first one !

About Regina Mkonde

error: Content is protected !!
Visit Us On FacebookVisit Us On TwitterVisit Us On YoutubeVisit Us On Instagram