MAMLAKA YA Udhibiti na Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imefungua dirisha la maombi ya leseni za muda mfupi kwa wamiliki wa mabasi yenye uwezo wa kubeba abiria 50, yanayotaka kwenda mikoa yenye uhitaji mkubwa katika kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).
Taarifa iliyotolewa hivi karibuni na SUMATRA inaeleza kuwa, ili mabasi hayo yapewe leseni hizo, yanatakiwa kufungwa mfumo wa kufuatilia mwenendo wa mabasi (VTS) na masharti mengine ya uombaji leseni yatazingatiwa.
Katika sharti lingine, wamiliki wa mabasi wanatakiwa kuuza tiketi kwa njia ya kielektroniki itakayowezesha abiria kukata tiketi kwa urahisi.
Katika hatua nyingine, SUMATRA imewataka abiria wanaotarajia kusafiri nyakati za sikukuu kukata tiketi zao mapema, pamoja na kutafuta taarifa sahihi za kiwango cha nauli kutoka katika mamlaka hiyo.
Leave a comment