Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto amjibu Msajili vyama vya siasa
Habari za Siasa

Zitto amjibu Msajili vyama vya siasa

Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi wa Chama cha siasa cha upinzani ACT-Wazalendo nchini Tanzania ameamua ‘kupuuza’ barua ya msajili wa vyama vya siasa na kwamba wanaendelea na ujenzi wa chama chao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam….(endelea).

Kiongozi huyo na mbunge wa Kigoma Mjini anayemaliza muda wake, ametoa kauli hiyo leo tarehe 17 Julai 2020, baada ya barua ya msajili kutaka chama hicho kujiandaa kupokea adhabu kutokana na ukiukwaji wa sharia ya vyama vya siasa.

Kwenye ukurasa wake wa twitter Zito ameandika “Msajili wa Vyama vya Siasa katuandikia tena barua ya kutaka kukichukulia hatua Chama chetu ACT-Wazalendo kwa sababu ambazo hazina msingi kabisa wa kisheria wala mantiki. Tumeamua kumdharau na kuendelea na shughuli za Ujenzi wa Chama! #KaziNaBata.”

Kwenye barua hiyo iliyoandikwa tarehe 14 Julai 2020 na kusainiwa Sisty Nyahoza, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa imeeleza kusudio lake la kutaka kukipa adhabu ACT-Wazalendo kwa kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa.

“Kutokana na ukweli kwamba, tangu mwaka 2018 ACT-wazalendo mmefanya vitendo kadhaa vya kukiuka sheria ya vyama vya siasa na msajili wa vyama vya siasa amekuwa akiwaasa muache kufanya hivyo, lakini hamzingatii ushauri wake,” imeeleza barua hiyo

Soma zaidi hapa

Msajili aikamia ACT-Wazalendo atishia kuifuta

“Msajili wa vyama vya siasa anakusudia kuwapa adhabu chini ya sheria ya vyama vya siasa, ili iwe fundisho kwenu na kwa vyama vya siasa vingine kuwa, ni muhimu kuheshimu Sheria za nchi ikiwamo sheria ya vyama vya siasa katika shughuli za kisiasa na vyama vya siasa, hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!