October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ubingwa ‘La Liga’ Madrid yatawazwa rasmi

Spread the love

KLABU ya Real Madrid ya Hispania jana ilitangwazwa mabingwa wapya wa Ligi kuu nchini humo (La Liga), baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Villarreal na kufikisha alama 86, ambazao haziwezi kufikiwa na timu yoyote kwenye Ligi hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu… endelea

Madrid inachukua taji hilo kwa mara 34 katika historia huku ikifuatiwa na Fc Barcelona nafasi ya pili yenye pointi 79 baada ya kupoteza kwenye mchezo wa jana dhidi ya Osasuna kwa mabao 2-1, huku kila timu ikibakiwa na michezo miwili.

Baada ya kutwaa ubingwa huo Madrid inabakiwa kuwa klabu inayoongoza kwa kutwaa kombe hilo mara nyingi nchini Hispania chini ya kocha wake Zinedine Zidane ambaye ametwaa taji hilo mara mbili.

Taji hilo linakuwa la 11 kwa kocha huyo toka alipoaanza kukinoa kikosi hicho Januari, 2016 na baadae kurejea tena Machi, 2019 na kuwa mmoja wa kocha mwenye mafanikio zaidi kwa kutwaa jumla ya mataji 11, klabuni hapo.

error: Content is protected !!