Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Michezo Yanga kushusha chuma kingine
Michezo

Yanga kushusha chuma kingine

Mhandisi Hersi Said, Mkurugezni wa uwekezaji Gsm
Spread the love

 

Klabu ya Yanga ipo mbioni hivi karibuni kumtambulisha mchezaji mwengine mpya atakayejiunga na timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao wa mashindano. Anaripoti Wiston Josia/ TUDARCo(endelea…)

Kikosi hicho ambacho kwa sasa kimekita kambi nchini Morocco, kikiwa na siku mbili toka kianze mazoezi jana Agosti 17, 2021.

Akizungumza na Azam TV, akiwa nchini Morocco, makamu Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ndani ya klabu ya Yanga Mhandisi Hersi Said, mchezaji huyo ni moja kati ya wachezaji wapya wawili ambao hawajaripoti mpaka sasa licha ya kutomtaja jina lake.

“Wachezaji wote wameshaudhulia isipokuwa wachezaji wawili Kharid Haucho atakayewasili siku ya alhamisiu lakini kutakuwa na mchezaji mwengine ambaye stamtaja kwa sasa.” Alisema kiongozi huyo

Kikosi hicho kimeweka kambi Jijini Marrakesh, Morocco kujiandaa na michuano ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ambapo Yanga itaanza kwenye hatua ya awali dhidi ya Rivers United ya nchini Nigeria.

Katika hatua nyingine, akizungumzia juu ya suala la jezi, kiongozi huyo alisema kuwa jezi zinazotumika kwa sasa ni kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao (Pre-Season), lakini hivi karibuni watakuwa na hafla maalum za utambulisho wa jezi mpya.

“Hizi ni jezi kwa ajili ya maandalizi ya msimu (Pre – season) na tutafanya tukio maalumu la uzinduzi wa jezi za msimu ujao.” Alifunguka Hersi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!