Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Wanadiplomasia, raia 2200 wahamishwa Afghanistan
Kimataifa

Wanadiplomasia, raia 2200 wahamishwa Afghanistan

Mullah Abdul Ghani Baradar
Spread the love

 

TAKRIBANI wanadiplomasia na raia 2,200 wamehamishwa kutoka Afghanistan kwa ndege za kijeshi wakati juhudi za kuwahamisha watu zikiendelea kushika kasi nchini humo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Uhamisho wa raia nchini Afghanistan unatokana na wasiwasi uliobuka, kufuatia wanamgambo wa Taliban.

Kundi la Taliban limesema, linataka amani, na limeahidi halitalipiza kisasi kwa maadui zake wa zamani, wakiilenga hasa Marekani na washirika wake wa Jumuiya ya Kujihami (NATO).

Aidha, utawala wa Taliban umeahidi kuheshimu haki za wanawake, lakini kwa mujibu wa mafundisho ya dini ya Kiislamu.

Hata hivyo, licha ya ahadi zote hizo, maelfu ya Waafghani hasa wale waliofanya kazi kwa ushirikiano na vikosi vya usalama vya kimataifa kwa zaidi ya miongo miwili, wanapanga kuondoka nchini humo.

Afisa wa usalama wa mataifa ya Magharibi amesema “tunaendelea kwa kasi kubwa na juhudi za kuwahamisha watu, hadi sasa hatujapata changamoto zozote na tumefanikiwa kuwahamisha zaidi ya wafanyikazi 2,200 maafisa wa usalama na Waafghani waliofanya kazi katika ofisi za ubalozi.”

Afisa huyo hata hivyo hakueleza ni lini safari za ndege za umma zinatarajiwa kuanza.

Hakuweza pia kuweka wazi idadi ya raia wa Afghanistan waliokuwepo kati ya watu hao 2,200 waliohamishwa kwa kutumia ndege ya kivita ya Marekani ya kubebea mizigo.

Naye waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza, Priti Patel amesema, tayari taifa lake limefanikiwa kuwahamisha watu wapatao 1,000 wakati Waziri Mkuu Boris Johnson akiahidi kufanya kila liwezakano kuepusha mzozo mbaya wa kibinadamu nchini Afghanistan.

Alisema, “tutafanya kila juhudi kuwasaidia wale waliousaidia ujumbe maalum wa Uingereza nchini Afghanistan, na pia tutasaidia kwa kila hali eneo pana la Afghanistan ikiwemo kuzuia mzozo wa kibinadamu.”

Baada ya Taliban kuchukua usukani, afisa mwandamizi wa kundi hilo amesema mmoja kati ya viongozi na waanzilishi wake Mullah Abdul Ghani Baradar amerudi nchini humo kwa mara ya kwanza baada ya kuwa nje kwa zaidi ya miaka 10.

Afisa huyo mwandamizi ameliambia shirika la habari la Reuters, viongozi wa Taliban watajitokeza kwa macho ya ulimwengu tofauti na miaka ya nyuma, ambapo walikuwa wakiishi kwa usiri mkubwa.

Wakati hayo yakiarifiwa, kundi hilo limeilipua sanamu ya kiongozi wa dhehebu la Kishia aliyepambana na Taliban wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Afghanistan katika miaka ya 90.

Sanamu ya Abdul Ali Mazari, mbabe wa kivita aliyeuawa na Taliban mnamo mwaka 1996 wakati wanamgambo hao walipochukua madaraka kutoka kwa wapinzani wao ililipuliwa.

Mazari alikuwa kiongozi wa Waislamu wachache wa dhehebu la Kishia waliopitia mateso makubwa chini ya utawala wa Taliban, waislamu waliokuwa wengi wa madhehebu ya Sunni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Raia Pakistan walilia haki siku ya Mshikamano Kashimir

Spread the loveRAIA wa Pakistani waishio nchini Tanzania wameadhimisha siku ya Mshikamano...

Kimataifa

Ramaphosa akiri tatizo la umeme Afrika Kusini kuathiri sekta ya madini

Spread the love  RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesema tatizo la...

Kimataifa

Idadi ya vifo tetemeko la ardhi yafikia 9000

Spread the love  IDADI ya vifo vilivyotokana na tetemeko la ardhi lililotokea...

Kimataifa

Tetemeko la ardhi Uturuki: Vifo vyaongezeka hadi 4,800

Spread the love  Idadi ya vifo vilivyotokana na tetemeko lililotokea jana Jumatatu...

error: Content is protected !!