March 2, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wizara ya Kilimo yapata pigo, watumishi watano wafariki ajalini

Spread the love

WATUMISHI watano wa Wizara ya Kilimo na Chakula, wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea Njirii, Manyoni mkoani Singida. Anaripoti Mwandishi Wetu, Singida … (endelea).

Ajali hiyo iliyohusisha gari ya wizara hiyo yenye namba za usajili STK 8925 na roli la mafuta la kampuni ya Mount Meru ya Rwanda.

Watumishi wote watano waliokuwemo katika gari hilo wanaume watatu na wanawake wawili wamefariki papo hapo.

Majina ya watumishi hao ni Stella Joram Ossano (39), Esta Tadayo Mutatembwa (36),  Abdallah Selemani Mushumbusi (53), Charles Josephat Somi na Erasto Mhina (43).

Miili ya Marehemu inasafirishwa kuelekea hospitali ya mkoa wa Dodoma.

error: Content is protected !!