December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mo aitwa Singida, wazee wataka kufanya yao

Spread the love

MFANYABIASHARA maarufu Mohammed Dewji ‘Mo’ ameombwa kwenda mkoani Singida ili apozwe machungu. Anaandika Mwandishi Maalum … (endelea).

Akizungumza na wanahabari kwenye viwanja vya CCM Singida baada ya kupatikana Mo, Mzee Juma Mwandoghwe amesema, wazee wanataka kumchinjia mbuzi na kufanya dua kutokana na kutendewa unyama wa kutekwa na watu wasiojulikana.

Mo ni mzaliwa wa Singida ambaye ameongoza jimbo hilo kwa miaka 10 (2005-2015).

Hata hivyo, haijafahamika kama Mo ataitikia wito huo.

Akiwakilisha wazee wenzake, Mzee Mwandoghwe amesema kuwa, Mo anapaswa kutulizwa na kupewa faraja.

Mzee Mwandoghwe amesema kuwa, Mo yupo Dar es Salaam kibiashara na Singida ndio nyumbani hivyo wanao wajibu kwa kijana wao aliyewahi kuwaongoza kwenye jimbo hilo la Singida Mjini.

Mzee Mwandoghwe ameeleza kulaani ukatili alikfanyiwa Mo na kueleza kuwa kitendo hicho ni cha kinyama.

error: Content is protected !!