Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Waziri Mulamula ashiriki mkutano wa Baraza la Mawaziri AU
Habari Mchanganyiko

Waziri Mulamula ashiriki mkutano wa Baraza la Mawaziri AU

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akishiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje la Umoja wa Afrika (AU) ulioanza leo Jijini Malabo, Equatorial Guinea.
Spread the love

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula ameshiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje la Umoja wa Afrika (AU) ulioanza leo Jijini Malabo, Equatorial Guinea. Anaripoti Mwandishi Wetu, Malabo… (endelea).

Kufanyika kwa mkutano huo ni utekelezaji wa maamuzi ya Mkutano wa 35 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika tarehe 6 – 7 Februari 2022 Jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Mawaziri wa Mambo ya Nje Mambo ya Nje wa Umoja wa Afrika (AU) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mkutano wao

Mkutano wa Baraza la Mawaziri ulitanguliwa na Mkutano wa Kisekta wa Mawaziri wanaoshughulika na Wakimbizi, Wahamaji na Majanga ya Kibinadamu uliofanyika kuanzia tarehe 23 – 24 Mei, 2022 Jijini Malabo.

Mkutano huo pamoja na mambo mengine, jukumu lake kubwa ni kuandaa Mkutano Maalum wa 16 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu majanga ya kibinadamu pamoja na masuala ya mapambano dhidi ya ugaidi na mabadiliko ya serikali yasiyozingatia Katiba unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 – 28 Mei, 2022 Jijini Malabo.

Akiongea wakati wa Ufunguzi wa Mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Bw. Moussa Faki Mahamat alisema kuwa mkutano huo ni mahsusi katika kujadili changamoto mbalimbali za majanga ya kibinadamu pamoja na mapambano dhidi ya ugaidi na mabadiliko ya Serikali yasiyozingatia katiba.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipata ufafanuzi kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Balozi Innocent Shiyo (kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz kabla ya kuanza kwa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje la Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Jijini Malabo, Equatorial Guinea

“Mkutano huu unafanyika wakati Afrika linapita katika changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na za majanga ya kibinadamu,” alisema Bw. Mahamat

Aidha, Bw. Mahamat aliongeza kuwa ugaidi bado ni changamoto na mabadiliko ya Serikali yasioyofuata misingi ya katiba ambayo yametokea miaka ya hivi karibuni yamerudisha nyuma taratibu za kidemokrasia katika chaguzi katika Bara la Afrika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata, Mitaa watakaoshindwa kusimamia usafi kukiona

Spread the love  WATENDAJI wa kata, mitaa na vitongoji na maofisa afya...

Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Spread the love  MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili...

Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni...

Habari Mchanganyiko

Uholanzi wampongeza Rais Samia kuimarisha vyombo vya habari, demokrasia

Spread the love  UBALOZI wa Uholanzi nchini Tanzania, umempongeza Rais Samia Suluhu...

error: Content is protected !!