Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Maisha Burudika Apple Music yasherehekea mafanikio ya Bara la afrika
BurudikaHabari

Apple Music yasherehekea mafanikio ya Bara la afrika

Spread the love

JUKWAA la muziki la Apple Music, linasherehekea uzuri wa kipekee na mandhari ya Bara la Afrika kupitia muziki katika Africa Month (Mwezi wa Afrika) unaokwenda sambamba na kampeni maalum ya Africa Is… yenye lengo la kuuenzi na kuutangaza ubunifu na vipaji vya muziki vya Kiafrika. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kampeni ya Africa Is… itawashirikisha mastaa kibao wa muziki kutoka nchi za Afrika Mashariki, Magharibi, Kati na Kusini ambapo wasanii wakubwa takribani 18 wataonesha maana halisi ya kuwa Mwafrika.

Miongoni mwa wasanii watakaoshiriki kwenye kampeni hiyo kutoka Afrika Magharibi ni pamoja na Rema (Nigeria), Moliy (Ghana) Basketmouth (Nigeria) Kelvyn Boy (Ghana), Prince Gyasi (Ghana) na Andrea Iyamah (Nigeria).

Kwa upande wa Afrika Mashariki, wasanii watakaoshiriki kampeni hiyo ni pamoja na Chimano (Kenya) na Hussein Suleiman (Uganda) huku nchi zinazozungumza Kireno zikiwakilishwa na Soraia Ramos (Cape Verde) na Eliana Murargy wa Msumbiji.

Nchi zinazozungumza Kifaransa zitawakilishwa na Ferre Gola (DRC), Serge Ibaka (DRC) na Chrystel (Ivory Coast) na upande wa Afrika Kusini ikiwakilishwa na Bongeziwe Mabandla, Uncle Waffles, Slikour, Nduduzo Makhathini na Wanda Lephoto.

Pia Apple Music watakuwa na vipengele vingine kama playlist za Editorial, Genre, Artist Essentials na Behind The Boards pamoja na Exclusive Home Sessions.

“Kwangu mimi, Afrika, kama ulivyo muziki wetu, ni tajiri, wenye rangi za kuvutia na mandhari nzuri. Tunajua namna ya kufurahi. Tunajua namna ya kuleta mwangaza wa burudani kwenye chumba chenye giza, huku tukiutunza utu wetu na muziki wetu.

“Najua kampeni hii haitoshi kuwakilisha muziki wote wa Afrika lakini ni kitu kikubwa sana,” alisema Rema, ambaye ni miongoni mwa washiriki kutoka Nigeria. http://music.apple.com/

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BurudikaMichezo

Kizz Daniel aunguruma na EP mpya ‘Thankz alot’

Spread the loveMKALI wa muziki nchini Nigeria, Kizz Daniel ametoa EP yake...

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Burudika

Piga makofi kwa Mr. Eazi …achomoka na ‘The Evil Genius’

Spread the loveMAKOFI kwa Mr Eazi! Staa wa Afropop, Mr Eazi ameachia...

Burudika

Kishindo cha Afro B katika “Wo wo wo” akiwa na Rich the Kid&Rimzee

Spread the loveSTAA ambaye alitambulishwa na ngoma maarufu, Afrowave ‘Drogba’, Afro B,...

error: Content is protected !!