Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Waziri mkuu azindua filamu ya the Royal Tour Ruangwa
Habari Mchanganyiko

Waziri mkuu azindua filamu ya the Royal Tour Ruangwa

Spread the love

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka Halmashauri za Wilaya nchini kuweka mipango ya kuibua fursa za utalii ili zinufaike na idadi kubwa ya watalii wanaoingia nchini baada ya hamasa iliyochechewa na Rais Samia Suluhu Hassan kupitia filamu ya The Royal Tour. Anaripoti Mwandishi Wetu, Lindi … (endelea).

Majaliwa alitoa agizo hilo jana tarehe 8 Julai, 2022 alipouongoza umati mkubwa wa wananchi wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi kutazama filamu ya The Royal Tour kwenye uwanja wa Wandorwa wilayani hapo.

Alisema filamu ya The Royal Tour ina nafasi ya kuimarisha shughuli za maendeleo katika mikoa yote nchini ukiwemo na mkoa wa Lindi ambao una vivutio vingi vya uwekezaji na utalii, hivyo kila wilaya itumie fursa hiyo kuainisha vivutio vilivyopo na kuvitangaza mfano viboko vyenye ualbino ambavyo vinapatikana wilayani Kilwa.

“Viboko hawa ni wa kipekee sana hawapatikani sehemu yoyote na ni kivutio kizuri cha utalii kwani unaweza kuwaita na wakaibuka juu na ukiwaambia wazame wanazama, hivyo Maafisa Utalii mlioko makao makuu ya wilaya ya Kilwa wekeni mpango mzuri wa kutangaza viboko hawa, ni kivutio kikubwa cha utalii”

Waziri Mkuu alisema Rais Samia moja ya mkakati yake ni kuboresha na kukuza uchumi na amewahakikishia Watanzania na ulimwengu kuwa Tanzania ni sehemu salama ya kuja kuwekeza na ametoa fursa za uwekezaji nchini.

Alisema katika ziara zake anazozifanya nje ya nchi moja kati ya ajenda yake ni kuwakaribisha wawekezaji katika sekta mbalimbali zikiwemo za viwanda, madini, biashara, utamaduni na sanaa.

Majaliwa alisema Rais amekuja na ubunifu wa kutangaza vivutio mbalimbali vilivyopo nchini kwa kupitia filamu ya The Royal Tour, hivyo aliwasisitiza Watanzania wakiwemo wananchi wa wilaya ya Ruangwa kuitumia fursa hiyo kwa kuibua miradi ya uwekezaji itakayowainua kiuchumi na kutengeza ajira hususan kwa vijana.

“Migodi mikubwa ya madini mbalimbali yakiwemo ya Bunyu (Graphite) inayotarajiwa kufunguliwa hivi karibuni katika wilaya yetu ni fursa ambayo wana-Ruangwa tunapaswa kuichangamkia kwa kuwekeza kwenye miradi ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali itakayowawezesha wageni kupata huduma muhimu za kijamii kama malazi, chakula na usafiri.”

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack alisema mkoa huo tayari umeanza kunufaika tangu filamu hiyo izunduliwe, ambapo idadi ya watalii imeongezeka pamoja na wafanyabiashara wanaoingia kwa ajili ya kutafuta maeneo ya uwekezaji.” Fursa za utalii na uwekezaji mkoani Lindi ni nyingi sana wananchi wanatakiwa kuzichangamkia.

Filamu ya kihistoria ya Royal Tour ilizinduliwa nchini tarehe 28 Aprili, 2022 Jijini Arusha, filamu hiyo, imechangia kuimarisha shughuli za utalii na kusaidia kutangaza urithi wa utalii uliopo Tanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!