August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ugonjwa uliomuondoa Bi Hindu watajwa

Chuma Selemani maarufu kama ‘Bi Hindu’

Spread the love

 

FAMILIA ya Muigizaji mkongwe nchini, Chuma Selemani maarufu kama ‘Bi Hindu’, imeweka wazi maradhi yaliyosababisha umauti wa mkongwe huyo kwenye sanaa ya uigizaji kuwa ni saratani ya mapafu. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Bi Hindu ambaye pia alikuwa mchambuzi wa masuala ya kijamii na kifamilia katika kituo cha Redio ya EFM ameripotiwa kufariki dunia leo tarehe 9 Julai 2022, asubuhi.

Kifo cha msanii huyo kimethibitishwa na mtoto wake Mwanaidi ambaye ameeleza kuwa Mama yake aliugua kwa muda mrefu na saratani iliyomshambulia mapafu.

Mwanaidi amesema kuwa Mama yake alikuwa akiuguzwa nyumbani “Mama tulikuwa tukimuuguza nyumbani ambapo alikuwa akisaidiwa kupumua kwa mashine ya Oxygen,” amesema.

Mwanaidi amesema kuwa Mama yake alikuwa mtu mashuhuri hivyo ni muhimu mashabiki zake na watanzania kwa ujumla wajue msiba huo ulipo na taratibu nyingine watazidi kutoa taarifa. Amesema msiba upo Magomeni mtaa wa Uweje.

error: Content is protected !!