July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Mkenda asema kauli mbiu, matamko hayaboreshi kilimo

Prof Adolf Mkenda, Waziri wa Elimu

Spread the love

 

WAZIRI wa Kilimo nchini Tanzania, Profesa Adolf Mkenda amesema kilimo hakiwezi kuendeshwa kwa matamko au kaulimbiu bali kwa kuendesha kilimo chenye tija. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Profesa Mkenda ameyasema hayo jana Ijumaa, tarehe 24 Septemba 2021, wakati wa uzinduzi wa Kituo Mahiri cha Usambazaji Teknolojia za Kilimo cha Nzuguni, Kanda ya Kati Dodoma.

Amesema bado kunachangamoto kubwa katika Kilimo kutokana na kuwepo kauli mbiu nyingi na matamko bila kuwepo na juhudi za uboreshaji kilimo.

“Hatuwezi kuwa na kilimo cha uhakika kwa kuwa na kaulimbiu nyingi au matamko.”

“Mmekuwa mkisikia Kilimo ni uti wa mgongo, mara siasa ni Kilimo, Kilimo cha kufa na kupona na Kilimo kwanza, kaulimbiu hizo haziwezi kutusaidia kuboresha kilimo cha uhakika na cheye tija,” amesema Profea Mkenda

“Ili tuweze kuwa na kilimo chenye tija ni lazima kuwa na mbegu bora zilizofanyiwa utafiti na kuwahamasisha wakulima kulima kilimo bora chenye tija na biashara badala ya kuwa na kilimo cha kujikimu,” amesema

Pamoja na mambo mengine, Prof. Mkenda ameitaka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), kujikitazaidi katika kufanya utafiti ambao utasababisha upatikanaji wa mbegu bora na kuwaongezea kipato wakulima.

“Kutokana na umuhimu serikali imeongeza bajeti katika taasisi ya utafiti kutoka Sh.7.3 bilioni hadi Sh.11 bilioni,” amesema

Kwa upande wake, Mkudugenzi Mkuu TARI, Dk.Geoffrey Mkamilo alisema lengo kubwa la TARI ni kuhakikisha wanafanya utafiti ambao utaboresha kilimo kutoka katika kilimo cha kujikimu na kuwa na kilimo chenye tija.

“Lengo la kuwa na vituo vya kusambaza teknolojia ni kuhakikisha tunafanya utafiki kwa kupata mbegu bora na zenye kumsaidia mkulima kutoka katika kilimo cha kujikimu na kuwa na kilimo chenye tija.

“Tumeanzisha pia vituo vya teknolojia ya kilimo ikiwa ni sebemu ya kurahisisha utoaji wa elimu ya mafunzo kwa wakulima pamoja na upatikanaji mbegu bora kwa haraka”ameeleza.

error: Content is protected !!