Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Michezo Simba walamba dili la milioni 800, mabasi matatu
Michezo

Simba walamba dili la milioni 800, mabasi matatu

Spread the love

 

KLABU ya Simba ya Dar es Salaam imesaini mkataba wa miaka minne na Kampuni ya Africarrier Group inayohusika na usambazaji wa magari ya kampuni ya Eicher nchini. Anaripoti Helena Mkonyi – TUDARCo … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kusaini mkataba huo, jana Ijumaa, tarehe 24 Septemba 2021, Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez amesema dili hilo lina thamani ya Sh milioni 800.

Aidha, amesema mkataba huo umeiwezesha timu ya wakubwa ya Simba SC na timu ya wanawake ya Simba Queens kila moja kupatiwa mabasi aina ya Eicher yenye uwezo wa kubeba abiri 35 kila moja ilihali timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17- (Simba U17) wakipatiwa gari aina ya costa.

“Mabasi haya ya Eicher Simba kila moja ni zaidi ya Dola za Marekani 200,000, lakini sisi Simba hatujatoa hata Sh moja kuanzia bima hadi gharama za usafiri hadi kutufikia. Simba tutagharamia dereva na mafuta pekee,” amesema.

Amesema mabasi hayo yatakayotumika kwa safari zote za Simba, yatakuwa na tangazo la Africarrier mbali na Sport Pesa ambao ni wadhamini wakuu.

Wakati Mkuu wa Kitengo cha Sheria cha Africarrier, Ngassa Mboje amesema mkataba huo utanufaisha pande zote mbili.

Amesema lengo la kampuni hiyo ni kuhakikisha Simba inakuwa timu kubwa Afrika kwa pande zote za wanawake na wanaume.

“Kutokana na mafanikio ambayo klabu hizi zimepata ikiwamo Simba Queens tumeona lazima na sisi kama kampuni ya usafiri kusaidia kukuza soka la Tanzania. Kupitia udhamini tutumie fursa hii kuwapongeza Simba Queens,” amesema.

Ameongeza kuwa udhamini wao umeenda sambamba na kauli mbiu ya Simba kuwa Simba nguvu moja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

Michezo

Ujanja ni kubeti na Meridianbet

Spread the love  JUMAPILI ya leo imekaa kihela hela sana ndani ya...

error: Content is protected !!