Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Watakaofiwa na wazazi St Anne Marie kuendelea kusoma bure
ElimuHabari

Watakaofiwa na wazazi St Anne Marie kuendelea kusoma bure

Wanafunzi wa darasa la tatu shule ya St Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam wakicheza wimbo wa akatambala ulioimbwa na msanii Saida Kalori, wakati wa mahafali ya 20 ya shule ya awali ya shule hiyo mwishoni mwa wiki.
Spread the love

MBUNGE wa Bukoba Vijijini, Dk. Jasson Rweikiza, amesema mwanafunzi ambaye atafiwa na wazazi wake wakati akiendelea na masomo kwenye shule yake ya St Anne Marie Academy hatafukuzwa shule kwa sababu ya kukosa ada. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza kwenye mahafali ya 20 kwa wanafunzi wa shule ya awali  yaliyofanyika kwenye viwanja vya shule hiyo, Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam.

Alisema wakati wa mlipuko wa ugonjwa Corona wazazi 46 wenye wanafunzi kwenye mtandao wa shule hizo walikufa kwa ugonjwa huo lakini hakuna hata mwanafunzi mmoja aliyefukuzwa shule mpaka sasa kwa kukosa ada.

“Nilisema wakati ule tulipopoteza wazazi 46 wakati wa Corona kwamba shule za St Anne Marie Academy hakuna mwanafunzi atakayefukuzwa baada ya mzazi wake kufa na kushindwa kulipa ada napenda kurudia na kusisitiza msimamo ni ule ule,” alisema na kuongeza

Mbunge wa Bukoba Vijijini, (CCM), Dk Jasson Rweikiza akimlisha keki mmoja wa wanafunzi wanaohitimu elimu ya awali ya St Anne Marie Academy, wakati wa mahafali ya 20 ya shule hiyo yaliyofanyika shuleni hapo Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga (CCM), Santiel Kirumba na kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Gladius Ndyetabura.

“Hata baada ya Corona vifo vipo na hakuna ajuaye kesho yake kwa hiyo hatufukuzi mtu hapa na kama mwanafunzi alikuwa shule ya msingi atamaliza darasa la saba bila kulipa ada na kama yuko sekondari atamaliza kidato cha nne bila kulipa ada,” alisema Dk. Rweikiza

Aidha, alisema siri ya mafanikio ya shule hiyo kitaaluma kila mwaka ni shule kuwa na mazingira mazuri ya wanafunzi kusomea ikiwemo maktaba ya kisasa na maabara iliyosheheni vifaa vya kutosha pamoja na  na walimu mahiri wenye kujua kazi yao.

Alisema wanafunzi wa bweni wamekuwa wakila milo mitano kwa siku wakati wale wa kutwa hupatiwa milo miwili hali ambayo imechangia utulivu wa wanafunzi na kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa.

“Ninapozungumzia umahiri wa wanafunzi wa St Anne Marie wote mmeshuhudia namna mwanafunzi wa shule alivyomudu kusoma hotuba ya kurasa nne kwa kingereza bila shida yoyote, hiyo ni kazi kubwa ya walimu hongereni sana,” alisema

Alisema shule imejitahidi kuweka miundombinu ya kisasa ya usalama wakiwemo walinzi 46 na mbwa wenye mafunzo kuwahakikishia wanafunzi usalama wanapokuwa shuleni hapo.

Wahitimu wa shule ya awali St Anne Marie Academy ya Mbezi Kimara kwa Msuguri Dar es Salaam wakionyesha mitindo ya mavazi wakati wa mahali ya 20 ya shule ya awali yaliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki.

“Hawa askari 46 tulio nao wamepata mafunzo ya kisasa kiasi kwamba hata ukitokea moto wako tayari kuuzima ndani ya dakika chache sana kwa hiyo wazazi msiwe na wasiwasi na watoto wenu kitaaluma na kiusalama hapa St Anne Marie Academy,” alisema

Kwa upande wake, mgeni rasmi ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga, Santiel Kirumba, alimpongeza Dk. Rweikiza kutokana na mchango anaoutoa kwenye sekta ya elimu nchini.

“Kuhusu ubora wa elimu sina wasiwasi na nyinyi kwasababu nimemaliza kidato cha nne hapa mwaka 2005 shule hii naijua. Nakumbuka tulivyolelewa kwa maadili ya hali ya juu na kuhimizwa kusali kila mara na miundombinu niliyoikuta imenishangaza sana mmepiga hatua kubwa hongera sana Dk. Rweikiza,” alisema

Aidha, aliwataka wazazi kuwalea watoto wao kwenye maadili ya dini kwa kuwakumbusha kusali kila wakati badala ya kuwaachia walimu pekee jukumu hilo.

Aliwataka wazazi ambao watoto wao wamemaliza shule ya awali kuwaacha watoto wao wasome shuleni hapo kutokana na uhakika uliopo kuhusu maadili na kufanya vyema kwenye taaluma.

“Sote tunajua huko majumbani maadili yameporomoka sana kwa hiyo wazazi wamepekeni watoto kwenye shule ambazo mnauhakika watakuwa salama kimaadili na watafanya vyema kitaaluma,” alisema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

error: Content is protected !!