December 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watatu wapoteza maisha ajali ya ndege Bukoba

Spread the love

WATU watatu kati ya 27 waliookolewa hadi sasa wameripotiwa kupoteza maisha katika ajali ya ndege ya Kampuni ya Precision iliyotokea Bukoba mkoani Kagera. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Vifo hivyo vimethibitishwa na taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji makao makuu Dodoma, P. E. Nzalayaimisi.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa jeshi hilo linaendelea na juhudi za kuokoa abiria wengine 16 waliobaki ndani ya ndege na kuwataka Watanzania kuendelea kuwa watulivu.

https://youtu.be/2EwivzgaJzs

Mkuu wa Mkoa wa Kagera amesema Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajia kuwasili eneo la tukio muda wowote kuanzia sasa.

Ndege ya Precision yenye mruko namba PW 494 ikitokea Dar es Salaam kwenda Kagera ikiwa na abiria 39 akiwemo mtoto mchanga, ilipata ajali na kutua ndani ya Ziwa Victoria umbali mdogo kutoka uwanja wa ndege wa Bukoba.

error: Content is protected !!