December 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watu 26 kati 43 waokolewa katika ajali ya ndege Bukoba

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila

Spread the love

 

MKUU wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila, amesema watu 26 wameokolewa kati ya 43 waliokuwa kwenye ndege ya Precision ambayo imepata ajali na kutumbukia Ziwa Victoria. Anaripoti Mwandishi Wetu, Bukoba … (endelea).

Chalamila amesema wote waliookolewa wamefikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera lakini hajaweka wazi kama ni majeruhi au wamepoteza maisha na kwamba taarifa ya kina itatolewa baadae kuhusu hali zao.

Mkuu huyo wa mkoa ameitaja ndege iliyohusika kwenye ajali kuw ni ATR 42 yenye namba za usajili 5H-PWF iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam akiwa na watu 43 kati yao abiria ni 29, wahudumu wawili na marubani wawili.

“Tumekwishafanikiwa kuokoa watu 26 na ambao wamepelekwa moja kwa moja kwenye Hospitali yetu ya Rufaa ya Mkoa na kwa mantiki hiyo tutapata taarifa ya kinakuhusu hali ya wenzetu ambao tumewaokoa kwenye ajali hiyo,” amesema Chalamila.

Ametoa taarifa hiyo leo Jumapili tarehe 6, Novemba, 2022 ambapo amewataka watanzania kuendelea kuwa watulivu wakati zoezi la ukoaji linaendelea.

“Zoezi linaloendelea hivi sasa ni kuivuta ndege na kuangalia kama tairi zimegusa chini tupate utaalamu mwingine wa kina tuweze kuipush iweze kutoka.

Amesema hadi sasa bado kuna mawasiliano kutoka ndani ya ndege kupitia marubani wa ndege hiyo.

error: Content is protected !!