Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanawake TPA walipia bima ya afya watoto 400
Habari Mchanganyiko

Wanawake TPA walipia bima ya afya watoto 400

Spread the love

 

WAFANYAKAZI wanawake wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), wamewalipia bima ya afya watoto 400 kutoka wilaya za Temeke, Ilala na Kigamboni jijini Dar es Salaam. Anaripoti Selemani Msuya, Dar es Salaam … (endelea).

Wanawake hao wametoa msaada huo uliolenga familia zenye maisha magumu, ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo ilifanyika Machi 8 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukabidhi bima hizo jana tarehe 14 Machi, 2022, Kaimu Meneja Rasilimali Watu wa TPA Dar es Salaam, Mwajuma Mkonga amesema wamesukumwa kusaidia watoto hao ikiwa ni sehemu ya wao kurudisha kidogo kwa jamii.

Mkonga amesema wafanyakazi wanawake, mwajiri wao na wadau mbalimbali wameshiriki kupata fedha ambazo zimeweza kulipia bima ya afya kwa watoto 400.

“Katika kuendeleza maadhimisho ya siku ya wanawake sisi wanawake wa bandari tumechangishana fedha kidogo ambazo zimeweza kulipia bima ya afya kwa watoto 400 wa wilaya ya Temeke, Ilala na Kigamboni,” amesema.

Kaimu Meneja huyo amesema Wilaya ya Temeke wamelipia watoto 200, Ilala 100 na Kigamboni 100, hivyo ni imani yao kuwa watoto hao watanufaika kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Amesema pamoja na kulipia bima kwa watoto hao wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa ambovyo vimegharimu Sh.milioni 5.

Jokate Mwegelo, Mkuu wa Wilaya ya Temeke

Amesema msaada huo ni sehemu ya wao kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kwenye kuresha huduma za afya.

Mkonga ametoa wito kwa wadau wengine kujitokeza na kusaidia jamii hasa yenye changamoto.

Naye Mlezi wa watoto waliopatiwa bima hizo, Fatma Mohammed amesema msaada huo utawasaidia kutatua changamoto ya matibabu kwa watoto anaowalea.

“Sijui niseme nini, furaha niliyonayo haina kifani, ninachoweza kuwalipa ni kumuomba Mungu awazidishie mlichotoa na mwakani mtoe tena. Mmetusaidia pakubwa,”amesema.

Kwa upande wake Kaimu Ofisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Temeke, Emma Komba amewapongeza wanawake wa TPA kwa kuipa Temeke kipaumbele na kwamba wamechagua sehemu sahihi.

Komba amesema zoezi la kuwapata watoto wahitaji limeenda vizuri ila wanaomba wadau wengine waendelee kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kupata bima.

“Tunawashukuru sana kwa msaada wenu kwani umeweza kusaidia familia zenye hali ngumu ya maisha, zikiwemo familia za mapacha,” amesema.

Komba amesema katika wanufaika wa bima hizo wapo pia wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Mbagala na Sandali.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Jokate Mwegelo amesema wanawake wa TPA wamefanya jambo kubwa ambalo linapaswa kuuungwa mkono, huku akiwaomba na mwakani kuwakumbuka tena.

Mwegelo amesema dhamira ya Serikali ni wananchi kupata huduma bora za afya hivyo walichofanya wanawake wa TPA ni ushuhidi tosha wa kuunga mkono juhudi za Serikali katika afya.

“Kusema ukweli hili mlilofanya linapaswa kuigwa na kila mpenda maendeleo, niwaombe mwakani tena mtukumbuke bado uhitaji ni mkubwa,”amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!