Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko GFA Vehicle yaiangukia Serikali, Dk. Kijaji awajibu
Habari Mchanganyiko

GFA Vehicle yaiangukia Serikali, Dk. Kijaji awajibu

Spread the love

 

KIWANDA cha kuunganisha na kutengeneza magari cha GFA Vehicle Assemblers, kimeiomba Serikali ya Tanzania kurekebisha sheria na kupunguza ushuru ili kuwalinda wawekezaji wazalendo kuweza kushindana na wawekezaji wakubwa kutoka nje ya nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Aidha, aliishauri serikali kuwaomba waagizaji wa magari (trucks) kuagiza vipuri na kazi ya uunganishwaji ifanyike nchi ili kuweza kuokoa fedha za kigeni ambazo zingetumika kwa kuagiza magari na badala yake kutanua soko la ajira kwa vijana.

Hayo yamesemwa na Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho, Ezra Mereng’ jana Jumatatu, tarehe 14 Machi 2022, wakati Kamati yaBunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ilipotembelea viwanda vya kuzalisha chanjo za mifugo nchini ( HESTER Biosciences Africa Ltd ) na GFA Vehicle Assemblers.

Alisema kiwanda hicho kipo katika awamu ya pili ya uzalishaji mpaka sasa kimetengeneza magari 420 kwa kipindi cha mwaka mmoja wa uzalishaji ambapo kazi nyingi katika kiwanda hicho hufanywa na Watanzania waliopata ujuzi kutoka kwa wataalamu wa kigeni.

Mareng’ alisema kiwanda hicho kina wafanyakazi zaidi ya 100 na kati yao 95 ni Watanzania na watano ni wageni kutoka nje ya mipaka ya Tanzania.

Akijibu baadhi ya hoja zilizotolwea na wawekezaji hao, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji aliwatoa hofu wawekezaji hao na akisema serikali ya awamu ya sita ipo karibu nao na suala la ukatikaji wa umeme ambalo ni miongoni mwa changamoto zilizowasilishwa inalifanyia kazi.

Dk. Kijaji alisema serikali ipo katika hatua za kuongeza vyanzo vya umeme mkubwa ikiwemo mradi wa umeme wa bwawa la Nyerere litakuwa mkombozi wa tatizo hilo.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Erick Shigongo alisema swala la kubadilisha sheria kumlinda mwekezaji wa ndani (local content) kamati itafikisha bungeni kwani wao ndio wenye mamlaka ya kutunga sheria hizo ili wawekezaji waweze kushindana katika soko na wawekezaji wakubwa kutoka nje.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

error: Content is protected !!