Wednesday , 1 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wanawake Chadema waingilia kati sakata la Pauline Gekul
Habari za Siasa

Wanawake Chadema waingilia kati sakata la Pauline Gekul

Spread the love

BARAZA la Wanawake la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA), wilayani Ilala, limeitaka Serikali kushughulikia kwa ukamilifu tuhuma za ukatili wa kijinsia, zinazomkabili aliyekuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Pauline Gekul, ili haki itendeke. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 30 Novemba 2023, jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa BAWACHA wilayani Ilala, Joyce Mwabamba aliyetoa tamko la baraza hilo la kulaani kitendo cha ukatili anachodaiwa Gekul kumfanyia aliyekuwa mfanyakazi wake, Hashim Ally.

“Sisi kama wanawake tuliopewa dhamana ya kulinda haki za wanawake na watoto, tunalaani vitendo hivi, ni aibu sana kwake sababu ni kiongozi hakustahili kushiriki kitendo hiko. Tunaitaka Serikali kupitia vyombo vyake vya dola, kusimamia jambo hili bila upendeleo na kwa uwazi huku tukiomba ulinzi kwa vijana hao ili ushahidi usipotee,” amesema Mwambapa.

Sakata hilo liliibuka baada ya kusambaa mtandaoni tuhuma za Gekul kuongoza watu wake kumfanyia ukatili kijana huyo, ikiwemo kumuingiza chupa sehemu za siri, akimtuhumu kutaka kumpa sumu na kumfanyia ushirikina katika hoteli yake anayoimiliki ya Palei Lake View Garden, iliyoko Babati.

Akihojiwa na moja ya televisheni ya mtandaoni, Ally alidai Gekul aliamuru watu wawili wamtese yeye pamoja na kijana mwingine aliyemtaja kwa jina la Michael, akiwatuhumu kwamba wanatumiwa na mpinzani wake kibiashara, Grace Shayo, kumpa sumu pamoja na kuroga biashara yake.

Gekul na Shayo ni wapinzani kibiashara ambao kwa pamoja wanauza chakula kwa abiria wa mabasi ya mikoani.

“Sisi tukasema hapana, mbona hatujatumwa akawa anatulazimisha tuseme kuwa tumetumwa huku akiturekodi kwenye simu yake anatulazimisha. Tukaendelea kusema kweli kuwa hatujatumwa, aliamuru wale watu wawili watupige na kututishia kuwa atatupiga bastola akatutupe ziwani,” alidai Ally.

Ally alidai kuwa, baada ya yeye na Michael kukataa kutumwa kumwekea sumu, Gekul aliamuru wavuliwe suruliali kisha wawekwe chupa katika sehemu za haja kubwa “tukaendelea kusema ukweli, bado akamuru tuvuliwe suruali na tuingizwe chupa katika sehemu zetu za haja kubwa.”

Baada ya sakata hilo kushika kasi, Gekul kpoitia katibu wake, Hussein Abrima, alitoa ufafanuzi akidai hakumfanyia ukatili kijana huyo, bali linachochewa na ndugu wa Shayo, Vaileyh Shayo, ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Babati.

“Wote wanaendelea kusambaza taarifa hizi zilizozua taharuki juu ya jambo hili, Kwa kuwa wanalipeleka kwenye mrengo wa kisiasa na kuchafua hadhi na jina la mheshimiwa,” imesema taarifa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!