Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Wanajeshi Kenya wauwawa katika shambulizi linaloshukiwa kuwa la Al-shabab
Kimataifa

Wanajeshi Kenya wauwawa katika shambulizi linaloshukiwa kuwa la Al-shabab

Spread the love

 

ZAIDI ya wanajeshi 10 wadaiwa kuuwawa na wengine watano kujeruhiwa katika shambulio la kilipuzi kilichotegwa kando ya barabara kusini mwa Somalia. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mlipuko huo ulitokea baada ya gari lao kukanyaga kilipuzi kilichotegwa katika eneo la Gedo , karibu na mpaka wa Kenya -Somalia border leo Jumatano .tarehe 16 machi 2022.

Aidha majina ya Wanajeshi hao, waliouwawa katika shamulio hilo bado hayajatolewa lakini mgombea wa zamani wa wa Urais nchini Kenya ameandika katika mtandao wa Twitter kwamba ndugu yake mdogo ni miongoni mwa waliofariki Dunia.

Hata hivyo, shambulio hilo limehusishwa na kundi la Al-Qaeda lenye uhusiano na Al-Shabab, ambalo limefanya mashambulizi hayo, dhidi ya raia na msafara wa vikosi vya usalama.

Wanajeshi hao waliouwawa ni miongoni mwa vikosi vya kulinda Usalama wa Muungano wa Afrika kilichopelekwa Somalia, kusaidia Serikali ya nchi hiyo kukabiliana na wanamgambo wa al -Shabab.

Hivi karibuni ,imeshuhudiwa ongezeko la mashambulizi yanayolenga maeneo ya umma , mitambo ya Serikali na vituo vya ukaguzi vya Usalama .

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!