Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wanafunzi 50 wapatiwa mafunzo kazini, 15 waula mgodini
Habari Mchanganyiko

Wanafunzi 50 wapatiwa mafunzo kazini, 15 waula mgodini

Spread the love

KAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imewaaga na kuwapatia vyeti wanafunzi 50 kutoka vyuo vikuu waliokuwa wanafanya kazi katika mgodi huo kupitia Mpango wa Mafunzo Kazini kwa mwaka 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Wanafunzi hao ambao 30 ni wa kike na 20 wa kiume, waliopokewa Februari mwaka jana, wameagwa mwishoni mwa iliyopita mkoani Geita.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), Terry Strong akimtunuku cheti Julieth Lwehabura – mmoja wa wanafunzi 50 wa vyuo vikuu walioshiriki katika programu ya mafunzo kwa vitendo kwa mwaka 2023. Wanaoshuhudia kushoto ni Meneja Mwandamizi Rasilimali Watu, Charles Masubi (kushoto) na Meneja wa Mafunzo na Maendeleo Dominic Marandu (kulia).

Hata hivyo, kati yao 15 wamefanikiwa kubaki ndani ya kampuni hiyo ambapo watano wamepatiwa mkataba wa kudumu huku 10 wakipatiwa mkataba wa muda chini ya taratibu za program hiyo ya wahitimu.

Hatua hiyo ni mwendelezo wa mpango wa GGML wa kuchukua wanafunzi wa vyuo vikuu na kuwapatia uzoefu wa kufanya kazi katika fani mbalimbali ndani ya mgodi huo kwa lengo la kuunga mkono mipango ya serikali ya kuimarisha uwezo wa wahitimu kuajiriwa.

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga wahitimu hao, mwishoni mwa wiki mkoani Geita, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong amewapongeza wanafunzi hao kwa kudumisha uweledi na juhudi katika kazi walizokuwa wakizifanya kwa kipindi cha mwaka mmoja ndani ya mgodi huo.

Amesema wanafunzi hao walikuwa wakijituma kwa bidii na kuonesha uwezo wao katika nyanja mbalimbali walizokuwa wamepangiwa na wasimamizi wao ndani ya GGML.

Aidha, amewaomba waende kuwa mabalozi wema katika kuitangaza GGML kwa yale mema yote waliyojifunza kipindi chote cha mwaka mzima.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), Terry Strong akimtunuku cheti Shamimu Mfinanga – mmoja wa wanafunzi 50 wa vyuo vikuu walioshiriki katika programu ya mafunzo kwa vitendo kwa mwaka 2023. Wanaoshuhudia kushoto ni Meneja Mwandamizi Rasilimali Watu, Charles Masubi (kushoto) na Meneja wa Mafunzo na Maendeleo Dominic Marandu (kulia).

Sambamba na hayo Terry amesema GGML itachukua wanafunzi 40 katika mpango huo wa kuwapatia mafunzo kwa mwaka huu wa 2024. Kati yao 20 watakuwa wa kike na 20 wa kiume.

Wakizungumza baada ya kumaliza mafunzo hayo, mmoja wa wanafunzi hao, Julieth Lwehabura ameishukuru GGML kwa kuwapokea na kuwapatia uzoefu wa kipekee ambao utakuwa chachu kwao katika kuendelea kupiga hatua katika taaluma zao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), Terry Strong akimtunuku cheti Magnusi Kamugisha – mmoja wa wanafunzi 50 wa vyuo vikuu walioshiriki katika programu ya mafunzo kwa vitendo kwa mwaka 2023. Wanaoshuhudia kushoto ni Meneja Mwandamizi Rasilimali Watu, Charles Masubi (kushoto) na Meneja wa Mafunzo na Maendeleo Dominic Marandu (kulia).

Naye Shamimu Mfinanga alisema uzoefu walioupata ndani ya GGML unakwenda kufungua milango ya fursa kwao hasa ikizingatiwa hiyo ni kampuni kubwa ambayo imejitolea kuwa mfano wa kuigwa kwa kuwajali wanafunzi wanaohitimu vyuo vikuu nchini.

Tangu kuanza kwa program hiyo mwaka 2009, GGML imeshatoa mafunzo kwa wanafunzi 218 kutoka vyuo mbalimbali kati yao wanawake 131 na wanaume 87.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!