Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Waliofukuzwa kwa vyeti feki kuanza kurejeshewa michango ya hifadhi ya jamii Novemba Mosi
Habari Mchanganyiko

Waliofukuzwa kwa vyeti feki kuanza kurejeshewa michango ya hifadhi ya jamii Novemba Mosi

Prof. Joyce Ndalichako
Spread the love

 

KUANZIA Novemba Mosi, 2022 utekelezaji wa ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwarejeshea michango yao wale wote waliofukuzwa kazi kwasababu ya vyeti feki, utaanza rasmi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dododma … (endelea).

Itakumbukwa kuwa katika sherehe za Mei Mosi mwaka huu Rais Samia aliahidi kuwarejeshea michango yao iliyokuwa ikikatwa katika mishahara yao pekee bila kuhusisha michango ya waajiri wao. Hii ina maanisha kuwa waliokuwa watumishi wa Serikali watarudishiwa asilimia tano huku sekta binafsi wakirudishiwa asilimia 10 ya mishahara yao.

Watumishi zaidi ya 14,000 walifukuzwa kazi kufuatia zoezi maalumu la kubaini wale wote waliopata ajira kwa udanganyifu wa vyeti lililofanywa na Serikali kwa msaada wa Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) kuanzia Oktoba 2016 hadi Aprili mwaka 2017.

Akizungumza na waandishi wa habario leo Jumatano tarehe 26 Oktoba, 2022, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Joyce Ndalichako, amewataka wahusika kuwasiliana na waajiri wao kwaajili ya kushughulikia suala hilo.

“Marejesho ya michango kwa watumishi hao yataanza kufanyika kuanzia tarehe 1, Novemba, 2022 na tungependa kwa kweli jambo hili likamilike ndani ya muda mfupi kwa hiyo ili kuwezesha malipo hayo kufanyika mtumishi husika atatkiwa kwenda kwa aliyekuwa mwajiri naomba wasiamkie kwenye Mifuko ya jami.

“Taratibu ni zilezile anatakiwa aliyekuwa mwajiri wake akiwa na nyaraka zifuatazo awe na picha mbili pasaport size awe na nakala za kibenki yaani kwenye akaunti iliyo hai malipo haya hayatolewi pesa taslimu yatafanyika kwenye benki kwa hiyo lazima mtumishi husika aonyeshe taarifa zake za kibenki lakini pia atatakiwa awe na kitambulisho” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!