December 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge CCM ashauri kuondoshwa Tozo kwenye Korosho

Mbunge wa Ndanda Cecil Mwambe

Spread the love

 

MBUNGE wa Ndanda Cecil Mwambe ameishauri Serikali kufuta tozo zilizokuwepo kwenye utaratibu za maozo ya kurosho ghafi ili kunusuru bei ya korosho ambayo imelalamikiwa na wakulima wa zao hilo Mtwara na Lindi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mtwara … (endelea).

Amesema kitendo cha serikali kupitia waziri wa Kilimo na Ufugaji Hussein Bashe kukiri kuwa bei ya korosho ghafi duniani imeshuka kinaondoa matumaini ya bei ya korosho ghafi nchini kupanda.

Mwambe amesema tishio jingine la soko la korosho ya Tanzania ni kufunguliwa kwa soko la Msumbiji mapema Novemba mwaka huu .

Waziri Bashe, amenukuliwa kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, akiieleza:-

“Gharama za uzalishaji kilo moja ya korosho ni Tsh.1,470.60″

Katika soko la Dunia bei ya korosho imeshuka, uzalishaji wa korosho ghafi Duniani umeongezeka kwa zaidi ya Tani 200,000 ambazo hazijapata soko, nyingi zikiwa kwenye soko la India na Vietnam…”

Mwambe anasema ametafakari hali hiyo na kuona njia pekee ya kumuokoa mkulima ni kupunguza tozo.

“Naishauri serikali kuharakisha kufanya uamuzi wa kuchukua hatua ya kuondoa baadhi ya tozo ili iweze kurudi kwa mkulima wa korosho na kujaribu kuziba pengo la harasa anayoweza kupata kutokana na kushuka kwa bei ya korosho mnadani” amesema.

Zao la Korosho

Amesema kuwa ili wakulima wasikate tamaa na warudi mashambazi msimu ujao serikali ichukue hatua za mapema.

“Ukiangalia soko la Mozambique korosho inakwenda kwa wastani wa dola 0.56 kwa mujibu wa waziri, sasa tukiendelea kusubiri mpaka Msumbiji wakafungua biashara /minada yao ya korosho, sisi tutaathirika zaidi kwa sababu ya wanunuzi wataacha kununua kabisa Tanzania na watakwenda Mozambique ambako kutakuwa na bei ya chini, na tunafahamu Mozambique hawana matozo mengi kama yalivyo hapa Tanzania”

Mwambe amependekeza na kupunguzwa kwa tozo hizo kwa kuwa hakuna dalali ya kupanda kwa bei ya korosho duniani.

Amesema kuwa kikotoo cha mauzo na tozo inamuacha mkulima akipata hasara .

Amesema kuwa gharama za uzalishaji ni kama wastani wa 1,470, tozo ni zaidi ya Tsh. 300 kwa hiyo mkulima atapata hasara kwenye gharama za awali za uzalishaji lakini ukiacha gharama za uzalishaji ambazo ni tsh. 1470, .

haipatikani na mkulima anaona anapata hasara, kutokana na gharama za uzalishaji sasa naishauri serikali iamue sasa kwa makusudi waondoe makato ili mkulima aweze kupata faida kidogo na aweze kusonga mbele na ajiandae na maandalizi ya shambani msimu unaofuata.

Anabainisha kuwa hoja ya wakulima kukataa kuuza korosho yao ni ya msingi kwa sababu kwa bei zilizopo mnadani ambayo bei ya juu ilikuwa Tsh. 2,200 na bei ya chini Tsh.1,480, hazimpi faida kutokana na kupanda kwa gharama za uzalishaji wa zao hilo.

“Kinachowafanya wakatae ni kitu halisi kabisa ukiangalia gharama za uzalishaji ni wastani wa Tsh.1470 kwa kilo, makato mbalimbali ni tsh.300 kwa hiyo mkulima akikubali kuuza kwa bei ya chini ya tsh. 1,480.

error: Content is protected !!