Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema
Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Wanachama Chadema wakiandamana
Spread the love

MIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori la mizigo na magari matatu, iliyotokea katika Barabara Kuu ya Arusha-Namanga Ngaramtoni Kibaoni, jijini Arusha, itaagwa kesho tarehe 27 Februari 2024, kwenye Uwanja Wa Sheikh Amri Abeid. Anaripoti Mwandishi Wetu. Arusha…(endelea).

Ratiba hiyo imetolewa leo tarehe 26 Februari 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella, akizungumzia hatua zinazoendelea kuhusu ajali hiyo iliyotokea Jumamosi iliyopita.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela

“Kesho kuanzia saa tatu asubuhi kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, kutakuwa na zoezi la kutoa heshima za mwisho kwa ndugu zetu ambao wanaenda kwenye kupumzishwa. Niwaombe wana Arusha tushirikiane katika zoezi hili la kutoa heshima za mwisho,” amesema Mongella.

Aidha, Mongella amesema shughuli ya kuaga miili hiyo haitaathiri maandamano ya amani yaliyopangwa kufanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

“Niwaombe tuvumiliane kwa kesho, rai yangu kuwaomba viongozi wenzetu wahakikishe hilo maandamano hayo ya hiari. Tunatambua uwepo wa maandamano ya Chadema yapo kisheria na yatasimamiwa kama maeneo mengine,” amesema Mongella.

Ajali hiyo iliyojeruhi watu zaidi ya 20, ilitokea Jumamosi jioni baada ya gari la kubeba mizigo lililokuwa linatokea Namanga kwenda Arusha, kugonga magari matatu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Askofu Shoo awataka ACT kupigania maslahi ya Taifa, wasikubali kuhongwa

Spread the loveALIYEKUWA Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, Askofu...

Habari za Siasa

Biteko aagiza waajiri kudhibiti vifo mahali pa kazi

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

error: Content is protected !!