Saturday , 4 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Tembo aongoza migongano binadamu, wanyamapori
Habari Mchanganyiko

Tembo aongoza migongano binadamu, wanyamapori

Spread the love

IMEELEZWA kuwa asilimia 80 ya migongano baina ya binadamu na wanyamapori nchini inahusisha mnyama tembo, huku simba, boko, mamba, fisi na nyati wakichangia asilimia 20. Anaripoti Selemani Msuya … (endelea).

Hayo yamesemwa na Ofisa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Isaack Chamba wakati akiwasilisha mada kwenye semina ya waandishi wa habari wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), mwishoni mwa wiki wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Mafunzo hayo yameandaliwa na JET kwa ufadhili wa Mradi wa Kupunguza Migongano Baina ya Binadamu na Wanyamapori unaotekelezwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) kwa niaba ya Serikali ya Ujerumani (MBZ).

Ofisa huyo amesema katika matukio zaidi ya 11,633 yaliyotokea kuanzia mwaka 2016 asilimia 80 yamehusisha tembo, ambapo ameweka wazi kuwa wananchi wameingia katika makazi ya wanayama.

Chamba ametaja wanyama wengine ni Simba asilimia 6, Kiboko asilimia 5, Nyati asilimia 4, Mamba asilimia 3 na Fisi asilimia 2.

Amesema mwaka 2016 hadi 2017 yametokea matukio 833, 2017/2018 matukio 997, 2018/19 matukio 1,510, 2019/20 matukio 1,426, 2020/21 matukio 1,706, 2021/22 matukio 2,304 na 2022/23 matukio 2,817, hiyo ikiwa ni ongezeko la asilimia 23.7.

Alitaja wilaya 10 zilizopata matukio mengi zaidi kuwa  Busega 226, Kilwa 221, Meatu 173, Nachingwea 163, Rufuji 155, Lindi 151, Manyoni 144, Tunduru 123, Bunda 105 na Itilima 100.

“TAWA tunaendelea kutoa elimu ya namna ya kukabiliana na changamoto ya migongano baina ya binadamu wanyamapori ila bado hali si nzuri kwani matukio yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka.

Ukifuatilia unagundua kwamba tembo ndio mnyama mwenye madhara zaidi, lakini ukichunguza zaidi ni kwamba wanadamu wamevamia makazi yao wanyama,” amesema.

Chamba amesema pamoja na wananchi kuvamia makazi ya wanyama, pia ipo changamoto ya mabadiliko ya tabianchi, kuingiliwa kwa shoroba, kukosekana kwa matumizi bora ya ardhi na mifugo kuingia kwenye hifadhi.

Mhifadhi huyo amesema katika kukabiliana na migongano hiyo mwaka 2022/2023 TAWA waweza kuua wanyamapori 108 ambao wameweza kuleta madhara kwa binadamu.

Alitaja baadhi ya wanyamapori waliouwa kwa kipindi hicho ni Tembo, Simba na Mambo ambao wakuwa wakitokea katika matukio mengi.

“Pia kuanzia 2017 hadi 2024 tumehamishia wanayama 65 kutoka eneo moja kwenda lingine ambapo Simba ni 63 na fisi wawili, lakini pia tumejenga vituo 16 ambavyo tumeweka polisi ili waweze kuongeza ulinzi,” amesema.

Aidha, Chamba amesema pamoja na kuongeza kasi ya usimamizi wa eneo hilo muhimu kwenye uchumi wa nchi, wametumia shilingi bilioni 9.6 kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi waozunguka maeneo yao.

Kwa upande wake Mtafiti kutoka GIZ, Dk Maria Montero amesema ili kuhakikisha migongano ya binadamu na wanyamapori ni lazima wadau wote kushiriki kwa kufuata sheria.

Dk Montero amesema kila mdau atasimama sekta ya uhifadhi kwa misingi ya sheria inawezakana kupunguza madhara ambayo yametokea kwa sasa.

“Kimsingi sisi wanadamu tumeingia maeneo ya wanyamapori, hivyo wakati wanyama wanarudi wanapatwa na mshangao na hapo migongano inatokea, amesema.

Mshauri wa GIZ Anna Kimambo ametoa rai kwa waandishi wa habari kuzingatia misingi ya uandishi ambayo inaenda kuleta mabadiliko na kusadia wadau wote.

Kimambo amesema GIZ wamekuja na mradi huo wa mwaka mmoja, ili kuhakikisha wanasaidia jamii kutambua madhara ya migongano iliyopo baina yao na wanyamapori.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!