Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko “Watanzania tembeleeni vivutio vya utalii”
Habari Mchanganyiko

“Watanzania tembeleeni vivutio vya utalii”

Hifadhi Saadan
Spread the love

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limewataka Watanzania kujitokeza kutembelea vivutio vya utalii ili kuongeza mapato ya ndani. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Wito huo umetolewa jana Jumapili na Kamanda wa Uhifadhi wa Kanda ya Mashariki, Gibril Mwishawa wakati akizungumzia hali ya uhifadhi nchini ambapo amewataka kuwa na utamaduni wa kutembelea hifadhi zilizopo nchini.

Mwishawa alisema Tanzania ina utajiri wa hifadhi na Tanapa wana Kanda nne za kiutawala kwa Kanda ya Mashariki ambazo ni Saadan, Nyerere, Mikumi na Udizungwa.

Akizungumza kuhusu hifadhi ya Sadaan ambapo wamefanya Tamasha la kuhamasisha utalii lililopewa jina la Aura 2024, alisema hifadhi hiyo ni muhimu kwa sababu ya kuwa na vionjo vya mbuga na bahari.

Alitaja sababu nyingine ya Watanzania kutembelea hifadhi hiyo kuwa ni kuchangiwa na kutembelewa sana na watalii na wageni, kama ilivyo kwa zile za Kaskazini.

Katika kuhakikisha hilo linakamilika amesema tayari wameshaainisha maeneo ya uwekezaji na yameshatumwa maombi mbalimbali ikiwemo na hifadhi ya Saadan kwa lengo la kusaidia kukuza utalii katika Hifadhi za Kanda za Mashariki.

Naye Kamishna msaidizi wa Maendeleo ya biashara Tanapa, Jully Lyimo akizungumzia kuhusu Sadaan alisema ni eneo zuri kwakuwa lina vivutio vya utalii wa kupanda gari, kuona wanyama, utalii wa kutembea, utalii wa usiku, utalii wa fukwe na boti.

Lyimo alitoa wito kwa Watanzania kutumia hifadhi hiyo ya Saadan, kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kipaimala, harusi na sherehe nyingine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!