Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wakili wa Selasini ajitoa kesi aliyofunguliwa na Mbatia
Habari za SiasaTangulizi

Wakili wa Selasini ajitoa kesi aliyofunguliwa na Mbatia

Joseph Selasini, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya NCCR Mageuzi
Spread the love

 

HASSAN Ruhwanya, Wakili wa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha NCCR-Mageuzi, Joseph Selasini, amejitoa kumuwakilisha katika kesi aliyofunguliwa na James Mbatia, akimtaka amlipe Sh. 10 bilioni, kama fidia ya kulichafua jina lake kwa kumtuhumu fisadi wa mali za chama hicho. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wakili Ruhwanya amewasilisha ombi hilo leo tarehe 13 Julai 2023, wakati kesi hiyo ya madai Na. 59/2023, ilipokuja kwa ajili ya usikilizwaji katika Mahakama Kuu, Masjala Kuu, jijini Dar es Salaam, mbele ya Jaji Mussa Pomo.

Wakili huyo amedai sababu za kuchukua uamuzi huo, ni baada ya mteja wake (Selasini), kumtaka ajitoe kwenye kumuwakilisha. Hata hivyo hajaeleza sababu za Selasini kumtaka afanye uamuzi huo.

Jaji Pomo alikubali ombi Hilo na kumtaka ampe taarifa ya wito Selasini, ili aje ahudhurie usikilizwaji wa kesi utakaoanza tarehe 16 Hadi 18 Agosti, 2023.

Jaji Pomo alipanga tarehe hizo, baada ya kuahirisha kesi kutokana na kushindwa kuendelea kwa kuwa Selasini hakutokea Mahakamani hapo na Wala hakutuma muwakilishi mwingine.

Mbali na Selasini, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya madai, ni kampuni za vyombo vya habari, ikiwemo Mwananchi Communication Limited, Wasafi media inayomilikiwa na msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma Issack (Diamond Platnumz).

Jamhuri Media Limited, inayochapisha gazeti la Jamhuri. Global Publishers na Mhariri wa Gazeti la The Citizens.

Miongoni mwa hoja za Mbatia, ni Selasini kumtuhumu kwa madai mbalimbali ikiwemo ni kibaraka wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameuza shamba la NCCR-Mageuzi lenye hekari 56 , kufuja nyumba za chama hicho, ambapo amemtaka kwenda mahakamani kuzithibitisha na kama akishindwa kuthibitisha amlipe fidia.

Kwa upande wa vyombo vya habari vilivyoshtakiwa, vinadaiwa kuchapisha tuhuma zilizotolewa na Selasini dhidi ya Mbatia. Vyombo hivyo na Selasini kwa pamoja wanashtakiwa na Mbatia anyetaka walimpe fidia ya pamoja kiasi cha Sh. 10 bilioni kama wakishindwa kuthibitisha tuhuma hizo.

Mbali na kesi hiyo iliyofunguliwa mahakama kuu, Mbatia amefungua kesi nyingine ya madai Na. 87/2023, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, dhidi ya Selasini, akitaka amlipe fidia ya kiasi cha Sh. 500 milioni.

Kwa madai amelichafua jina lake kwa kumtuhumu kuwa amewaomba rushwa ya Sh. 50 kila mmoja, waliokuwa wagombea viti maalum kupitia NCCR-Mageuzi, akiwemo Susan Masele.

Kesi hiyo imepanga kusikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

error: Content is protected !!