Tuesday , 26 September 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Ubongo yatimiza miaka 10, yawafikia makazi mil 32 Afrika, nchi 22
ElimuHabari MchanganyikoMichezo

Ubongo yatimiza miaka 10, yawafikia makazi mil 32 Afrika, nchi 22

Spread the love

 

KAMPUNI ya Ubongo inayozalisha vipindi vya elimu burudani Afrika, ina furaha kuwatangazia maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake, ikisherehekea muongo mmoja wa kuleta mabadiliko katika elimu na kuwawezesha mamilioni ya watoto katika bara hili ambapo imefanikiwa kuwafikia katika makazi milioni 32 katika nchi 22 za barani Afrika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Kupitia mkusanyiko wa programu za elimu zinazovutia ikiwemo Akili and Me, Ubongo Kids, bila kusahau Nuzo and Namia iliyoanzishwa hivi karibuni, Ubongo imeendelea kuwa kinara katika nyanja ya ubunifu katika ujifunzaji wa watoto.

Ubongo pamoja na kuwafikia idadi kubwa ya watu barani Afrika lakini bado wana mango wa kuwafikia idadi kubwa zaidi ambapo katika mikakati yao wanatarajia kuwafikia watu katika makazi milioni 60 ifikapo mwaka 2025 na makazi milioni 100 itakapofika mwaka 2028.

Tangu kuanzishwa kwake Julai 2013 hapa Dar es Salaam, Tanzania, Ubongo imejikita katika kutengeneza maudhui ya elimu yenye kufurahisha, kuelimisha na yenye kuzingatia lugha na tamaduni za Kiafrika zinazomfanya mtoto apende kujifunza. Kupitia teknolojia mbalimbali kama vile TV, redio, na simu za mkononi, Ubongo imeweza kufikia familia zaidi ya milioni 32 barani Afrika, na kufanya athari kubwa katika sekta ya elimu ya bara hili.

Mwanzilishi wa Ubongo, Cleng’a Ng’atigwa

Tafiti huru zilizochunguza programu za Ubongo zimeonesha mara kwa mara matokeo mazuri kama vile:  kuboresha utayari wa mtoto kuanza shule na viwango vya ujifunzaji, na kuchangia mabadiliko chanya ya kijamii na kitabia kwa watoto na walezi wao.

Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, Ubongo imekua kutoka shirika dogo la Tanzania hadi shirika lisilo la kiserikali lenye uwakilishi wa kina barani Afrika na kuwa kinara katika elimu-burudani barani Afrika. Programu za Ubongo zilizojaa ubunifu na zenye kusisimua, zinawawezesha watoto kupata maarifa na stadi muhimu zinazowasaidia kubadili maisha yao na jamii zao kwa ujumla.

“Tunafurahi kusherehekea hatua hii kubwa ya miaka 10,” alisema Mwasi Wilmore, Mkurugenzi Mtendaji wa Ubongo na kuongeza. “Huu ni ushuhuda wa kazi ngumu, uaminifu, na shauku ya timu yetu, washirika wetu, na wafuasi wetu ambao wameamini katika lengo letu na kuchangia mafanikio yetu.

“Pamoja, tumeweza kufanya mabadiliko makubwa katika elimu barani Afrika, na tuko na azma ya kuendelea na safari yetu ya kuleta mabadiliko katika ujifunzaji wa watoto kwa vizazi vijavyo.”

Rajabu Semtawa, Mwanzilishi wa Ubongo (katikati)

Kuadhimisha hatua hii muhimu, Ubongo imeandaa tukio maalum la kusherehekea miaka 10 hapa Dar es Salaam, litakalowakilisha mafanikio na hatua zilizofikiwa katika kipindi cha miaka yote hiyo. Tukio litajumuisha hotuba za kuvutia na mawasilisho ya kusisimua yakionyesha safari na athari za programu za Ubongo.

“Tunawaalika washirika wetu, wafuasi wetu, na wadau wote kuungana nasi katika kusherehekea hatua hii muhimu,” aliongeza Mwasi Wilmore. “Pamoja, tuweze kutafakari safari yetu, kutoa shukrani zetu, na kuendeleza dhamira yetu ya kutoa elimu bora na mabadiliko katika ujifunzaji wa watotou barani Afrika.”

“Tukiangalia miaka kumi ijayo, tunatazamia kusimama imara katika dhamira yetu ya kuwafikia watoto wengi zaidi, tukitumia nguvu ya  elimu-burudani kuwawezesha kufikia uwezo wao na kujenga mustakabali bora  wa bara la Afrika,” aliongeza Mwasi Wilmore.

Iman Lipumba, Mkurungezi wa Masoko Ubongo

Hafla hiyo ilihudhuriwa na baadhi ya mwanzilishi wa programu hiyo akiwemo Cleng’a Ng’atigwa ambaye ndiye aliyekuwa na wazo la kuanzisha katuni zenye maadili ya kitanzania pamoja na lugha ya kiswahili, anasema wazo hilo lilianza kichwani kwake miaka 23 iliyopita na anashukuru 2013 lilianza na leo limetimiza miaka 10.

Pia alikuwepo Rajabu Semtawa ambaye ni mmoja ya waanzilishi wa katuni hizo aliyeshiriki katika kutengeneza katuni hizo katika mfumo wa vibonzo vinavyoongea na kutembea (Amination), alisema wanafurahi ndoto zao zinaendelea kuishi hadi sasa.

Mbali na waanzilishi hao walishiriki pia Mohamed Kingara ‘Anko Zumo,’ Maisara Mohamed ‘Mai Zumo’ na Mary Nyadoi kutoka Uganda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Rais Samia apewa tano ujenzi barabara Mtwara

Spread the loveWANANCHI wa Mkoa wa Mtwara, wameishukuru Serikali ya Rais Dk....

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kununua mitambo 15 ya kuchoronga miamba

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Madini imepanga kununua mitambo 15 ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Mtanzania aweka rekodi kimataifa kwa kiwanda cha kusafisha dhahabu

Spread the loveIMEELEZWA kuwa Kiwanda cha Kusafisha dhahabu cha Geita Gold Refinery...

Elimu

Green Acres kuwakatia bima wanafunzi wote

Spread the loveShule ya Green Acres imejipanga kufanya mambo makubwa kwa mwaka...

error: Content is protected !!