Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wahariri waombwa kuhamasisha habari za uhifadhi wa bioanowai
Habari Mchanganyiko

Wahariri waombwa kuhamasisha habari za uhifadhi wa bioanowai

Spread the love

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), kimetoa raia kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini kuhamasisha waandishi kuandika habari za uhifadhi wa bioanowai. Anaripoti Selemani Msuya…(endelea).

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa JET, Dk Ellen Otaru wakati akizungumza na wahariri wanaoshiriki mafunzo ya siku mbili kuhusu hifadhi ya bioanowai kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, mafunzo yanayoratibiwa na JET na kufadhiliwa na USAID Tuhifadhi Maliasili.

Amesema lengo la JET kukukutana na wahariri ni katika kuhakikisha wanakuwa na uelewa wa mambo ya uhifadhi wa bioanowai na mazingira, hali ambayo itawafanya wahamasishe waandishi kuandika habari hizo kwa wingi.

“JET imetoa mafunzo ya uhifadhi wa bioanowai kwa waandishi wa habari, hivyo katika kuhakikisha jambo hili linakuwa ajenda ya vyombo vya habari tumelazimika kuwapa mafunzo wahariri ili nao wapate uelewa na wanapoletewa kazi za uhifadhi wazipe kipaumbele,” amesema.

Mwenyekiti huyo amesema JET inaamini iwapo wahariri watafundishwa faida za bioanowai watakuwa sehemu ya kampeni ya kufanya mazingira na shoroba yawe salama na endelevu.

Amesema jamii inahitaji kupata taarifa sahihi kuhusu uhifadhi wa bioanowai na mazingira, hivyo kupitia mafunzo hayo kwa wahariri wanaamini lengo litatimia.

Dk Utaru amesema wahariri na waandishi wanapaswa kuelimisha jamii kuwa suala la uhifadhi wa bioanowai na shoroba ni jukumu la kila mtu kwani madhara yake hayachagui.

Mjumbe wa Bodi ya JET, Bakari Kimwanga amesema chama hicho kupitia ufadhili wa USAID Tuhifadhi Maliasili wanatekeleza mradi katika shoroba saba, hivyo wanaomba waandishi na wahariri kuwaunga mkono katika kampeni hiyo inayolenga kulinda rasilimali za nchi.

Kimwanga amesema ombi la JET kwa wahariri kutoa kipaumbele kwa kila habari inayohusiana na uhifadhi wa bioanowai ambayo itawasilishwa kwenye dawati.

“Ninachowaomba ndugu zangu habari yoyote ya uhifadhi wa bioanowai msiiache kwani hali ni mbaya kwa sasa na sisi JET tutandelea kukutana nanyi ili tukumbushane,” amesema.

Mkurugenzi w JET, John Chikomo amesema ushirikiano ambao wanapata kwa vyombo vya habari umechangia wafadhili wa mradi ambao ni Marekani kuahidi kuwapatia fedha za utekelezaji.

Chikomo amesema mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili unapaswa kupongezwa kwa kuwa umeanza kutoa matokeo chanya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

error: Content is protected !!